![]() |
Rais Jakaya Kikwente na Ban Ki Moon |
NA MWANDISHI MAALUM, NEW YORK
Wakati watanzania wakiadhimisha hapo kesho miaka 47 ya Muungano.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amemtumia salamu za pongezi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, Serikali na watanzania wote.
Katika salamu zake ambazo nakala yake ilitumwa katika Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon anasema , wakati huu kuliko ilivyokuwa wakati mwingine wowote, dunia inakabiliwa na changamoto nyingi.
Amesema changamoto hizo ambazo zimevaa sura tofauti na uzito tofauti, zinavuka mipaka kutoka taifa moja hadi lingine. Na kwamba kuzitafutia ufumbuzi kunataka utulivu, umakini, mshikamano na ushirikiano wa kimataifa .
Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, amemwelezea Rais Jakaya Kikwete kwamba, yeye binafsi amedhamiria katika kuhakikisha kuwa Umoja wa Mataifa, unakwenda sambamba na kasi ya mabadiliko yanayotokea hivi sasa duniani. Na kuhakikisha kwamba Umoja wa Mataifa unasimamia na kutoa matarajio yenye kuridhisha na halisi katika kazi zake tatu kuu za msingi ambazo ni maendeleo, amani na usalama na haki za binadamu.
Ameeleza kuwa anafarijika na kutiwa moyo sana na uongozi unaojituma wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . Na kwamba anaihesabu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama mshirika mkubwa katika kuifanya dunia kuwa endelevu na salama kwa watu wote.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)