LUKAZA BLOG

Slider

KITAIFA

BIASHARA

FILAMU

AFYA

BURUDANI

MICHEZO

JAMII

Kamati ya Bunge yakoshwa na utendaji wa Benki ya NMB

NMB%2Bvs%2BKamti%2B5
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB - Ineke Bussemaker akizungumza katika kikao baina ya uongozi wa benki hiyo na Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma Juzi. Na Mpigapicha Wetu


NMB%2Bvs%2BKamati%2B2
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB - Ineke Bussemaker akizungumza katika kikao baina ya uongozi wa benki hiyo na Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma Juzi. Na Mpigapicha Wetu


NMB%2Bvs%2BKamati%2B6
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker akizungumza katika kikao baina ya uongozi wa benki hiyo na Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma Juzi. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Raphael Chegeni. Na Mpigapicha Wetu 

·        Faida ya NMB ya Shilingi billion 93.5 ni sawa na theluthi moja ya jumla ya faida ya mwaka ya benki zote nchini
·        Wabunge wapendezwa na mpango wa kuongeza mikopo kwa sekta ya kilimo

KAMATI ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma imeelezea kufurahishwa kwake na utendaji wa Benki ya NMB na kuahidi kufanya kazi pamoja na taasisi hiyo ya fedha ili kuendeleza uchumi wa nchi.

Akizungumza katika chumba cha mikutano kilichopo ndani ya Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni muda mfupi baada ya kuhudhuria semina iliyoandaliwa na NMB, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dk Raphael Chegeni alisema taarifa zinaonyesha benki hiyo imefanya vizuri katika nyanja zote.

“Kamati imefurahishwa na utendaji wa NMB na tumewataka waendelee kuwa wabunifu na kuboresha zaidi huduma kwa wananchi. Tumewataka waangalie zaidi sekta ya kilimo ambayo kwa mwaka jana ilipata asilimia tatu (3) tu ya mikopo yote iliyotolewa na benki za biashara kwa sekta mbali mbali za uzalishaji mali nchini,” alisema Dk Chegeni.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa NMB kwa Kamati hiyo ya Bunge inaonyesha kuwa idadi ya wateja wa benki iliongezeka kwa asilimia 24 kutoka milioni 2.179 kwa mwaka 2016 na kufika milioni 2.7 mwaka jana.

Idadi ya mashine za kutolea fedha (ATMs) ziliongezeka kutoka 670 mwaka 2016 na kufika 770 mwaka jana huku idadi ya matawi yakiongezeka kutoka 188 na kufika 212 mwaka jana kabla ya kufika 220 hivi sasa.

Benki ya NMB pia imefanikiwa kuongeza idadi ya mawakala wake (NMB Wakalas) kutoka 785 mwaka 2016 na kufika karibu 4000 mwaka jana kabla ya kuongeza zaidi kufika 6000 hivi sasa.

Thamani ya mali za benki iliongezeka kwa asilimia 11 kutoka Shilingi trililioni 4.95 mwaka 2016 na kufika Shilingi trilioni 5.5 mwaka jana huku amana za wateja zikipanda kwa asilimia 14.

Mwaka jana, NMB ilipata faida ya baada ya kodi ya Shilingi bilioni 93.5 ambayo ni sawa na theluthi moja ya faida ya benki zote za biashara nchini kwa pamoja (NMB ikiwemo) ambayo ilikuwa jumla ya Shilingi bilioni 286.

Kutokana na faida hiyo, NMB imetoa gawio la jumla ya Shilingi bilioni 32 kwa wanahisa ambapo serikali – ambayo inamiliki asilimia 31.8 ya hisa za NMB – imepata mgao wa Shilingi bilioni 10.17.

Akizungumza baada ya Dk Chegeni, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi Ineke Bussemaker, alisema mazungumzo kati uongozi wa benki yake na Kamati ya Bunge yalikuwa mazuri na kuahidi kuyafanyia kazi mambo mengi yaliyopendekezwa na watunga sheria hao.

“Tumepokea ushauri mzuri sana kuhusu ni maeneo gani Wabunge wangetaka tupeleke nguvu zetu zaidi…Tukitilia mkazo katika kilimo tutaweza kuwafikia wakulima wengi zaidi nchini kote,” alisema Bi Bussemaker.

Mbali na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, wengine waliohudhuria semina hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Bi. Hawa Ghasia na makamu wake Bw. Jitu Soni.

Wengine ni: Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali, Bi. Naghenjwa Kaboyoka, Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria Ndogo, Bw. Andrew Chenge na Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Bw. Peter Serukamba.

NMB TAWI MLIMANI CITY WAKIZAWADIA KITUO CHA YATIMA

IMG_0177Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mlimani City, Seka Samuel Urio (kulia) akimkabidhi Mamamlezi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Umra, Zamda Idrissa  (kushoto) sehemu ya msaada waliotoa katika kituo hicho. Misaada iliyotolewa  ni pamoja na mchele kg 100, maharagwe kg 50, sukari kg 50, mafuta ya kula lita  20, mbuzi wawili, sabuni za kufuli na dawa za meno katoni moja moja.

IMG_0182


Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mlimani City, Seka Samuel Urio (kulia) akimkabidhi mbuzi wawili Mratibu wa Kituo cha Watoto Yatima cha Umra, James Gabone (kushoto) ikiwa ni sehemu ya msaada waliotoa kwa watoto wa kituo hicho 
IMG_0199
Picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano ya msaada huo.

WAFANYAKAZI
 wa Benki ya NMB Tawi la Mlimani City jana walikitembelea kituo cha 
watoto yatima cha UMRA kilichopo Magomeni Mikumi na kuwazawadia watoto wa kituo hicho zawadi mbalimbali ikiwemo vyakula katika mfungo wa Ramadhani na vitakavyotumika katika Siku Kuu ya Idd mara baada ya mfungo mtukufu wa Ramadhani. Akizungumza wakati akikabidhi misaada hiyo, Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mlimani City, Seka Samuel Urio alisema msaada huo ni michango ya wafanyakazi wa benki hiyo katika tawi lake, ikiwa ni utaratibu wa kawaida kurejesha fadhila kwa wateja wao.

Alisema waliamua kukitembelea kituo hicho baada ya kuguswa na shughuli za kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu zinazofanywa na kituo hicho kilichopo Magomeni, Mikumi jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa vyakula vilivyotolewa na wafanyakazi hao ni pamoja na mchele kg 100, maharagwe kg 50, sukari kg 50, mafuta ya kula lita 20, mbuzi wawili, sabuni za kufuli na dawa za meno katoni moja moja.

"...Huu ni utaratibu wa kawaida kwetu kutembelea, kujumuika na kusaidia jamii hasa wenye uitaji, leo tumewazawadia watoto hawa wa kituo cha Umra vitu mbalimbali pamoja na vyakula vya mfungo wa ramadhani na vingine katika siku kuu ya Iddi inayokaribia mara baada ya kumalizika mfungo wa Ramadhani," alisema Urio.

Kwa upande wake Mratibu wa Kituo cha Watoto Yatima cha Umra, James Gabone aliishukuru Benki ya NMB kwa kutoa msaada huo ambao utasaidia watoto wao kupata chakula sasa na baadaye kwenye Siku Kuu ya Iddi, ambapo watoto huitaji faraja zaidi.

Aliziomba taasisi na watu wengine kukumbuka kuwasaidia watoto wanaoitaji msaada hasa waliopo katika mazingira hatarishi ili kujenga uhusiano mzuri na Mungu.

"...Unajua unapomsaidia muhitaji yeyote unajenga misingi ya upendo suala ambalo linasisitizwa sana na Mungu katika dini zote, tukipendana tutasaidiana na kuendeleza mahusiano mazuri na Muumba," alisema Gabone.

NOTISI KUTOKA MAMLAKA YA MAWASILIANO TUNALAZIMIKA KUSITISHA HUDUMA


MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU AIPONGEZA HOSPITALI YA MAMC-MLOGANZILA KWA KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  (mwenye kilemba cha bluu) anayemfuatia ni Makamu Mkuu wa Chuo, Huduma za Hospitali, Prof. Said Aboud wakipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa magonjwa ya dharula Dkt. Catherine Shali wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu,  Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  (mwenye kilemba cha bluu) akipata maelezo katika mashime ya MRI wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  (mwenye kilemba cha bluu) akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila jijini Dar es Salaam. Pembeni kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Huduma za Hospitali, Prof. Said Aboud.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  (mwenye kilemba cha bluu) akipanda ngazi za umeme.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  (mwenye kilemba cha bluu) na Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kulshoto) wakimsikiliza Mkuu wa Skuli ya Meno-MUHAS Dkt. Elison Simon wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akitoa maelekezo kwa Meneja wa Maabala Glory Mmbando wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa wakuu wa vitengo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Amani Ahmada mwenye umri ya miaka 6, wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na wafanyakazi wa hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila wakati wa ziara yake iliyofanyika leo.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili ( MUHAS), Andrea Barnabas Pembe akizungumza na wafanyakazi wa hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila wakati wa ziara yake iliyofanyika leo.
Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha akizungumza machache.
Wafanyakazi wakimsikiliza kwa makini.
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza kutolea machache ufafanuzi.

Picha ya pamoja na uongozi wa hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila.
Picha ya pmoja na wafanyakazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwasikiliza wananchi wanaopata huduma ya matibabu Mloganzila wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Huduma za Hospitali, Prof. Said Aboud akitolea ufafanuzi malalamiko ya wananchi wanaopata huduma katika hospitali ya Mloganzila.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameupongeza ungozi wa hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila kwa juhudi wanazokabialiana nazo katika kutatua changamoto wanazokabilia nazo.

Mhe. Suluhu ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila.
Makamu wa Rais amesema kwa vifaa vya kisasa vya umeme vilivyopo hospitalini hapo havipaswi kupata umeme wa mashaka .

Makamu wa Rais amesema kuwa wananchi wengi hawajajua umuhimu wa kuwa na bima ya afya hivyo elimu zaidi itolewe ili wananchi wengi wachangie huduma ya afya kwa kupitia bima zao hii itawapunguzia gharama sana wakati wa matibabu.

Makamu wa Rais aliutaka uongozi wa Mloganzila kutangaza kwa wananchi huduma zinazopatikana hospitalini hapo ambapo wana vifaa vya kisasa kabisa kwa ajili ya uchunguzi wa afya, Makamu wa Rais alisema huduma ya kupima saratani ya matiti katika hospitali ya Mloganzila ni shilingi elfu 30 tu.

Akiongea na Watumishi wa hospitali hiyo Makamu wa Rais amesema “ Mnaofanya kazi sekta ya afya mnafanya kazi ya Uunguzi na kujitolea malipo yetu yapo kwa mwenyezi Mungu”

Makamu wa Rais pia aliwasikiliza wananchi waliofika kwenye kupata huduma hospitalini hapo na kusema kuwa Serikali itajitahidi kushughulikia changamoto zinazojitokeza lakini aliwahimiza wananchi kuhakikisha wanakuwa na bima ya afya.

Mapema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alimuambia Makamu wa Rais kuwa (MAMC) Mloganzila ni kati ya hospitali saba zinazomilikiwa na serikali ambazo zinatoa huduma za matibabu ya kibingwa ngazi ya juu pia alimpongeza Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa kuweka msukumo wake katika huduma ya mama na mtoto ambapo juhudi za Makamu wa Rais zimezaa matunda ambapo leo hii kuna vituo 208 vimeboreshwa na kutoa huduma

JAMII ISHIRIKISHWE MABADILIKO TABIA NCHI KUWA NA KILIMO CHENYE TIJA

 Mshehereshaji wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi, Mtafiti mshiriki wa ESRF, Abdallah Henku akitoa utambulisho wa wanenaji wa mdahalo huo uliofanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa ESRF.
 Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Meneja ushirikiano, uragibishi wa sera kutoka taasisi ya Food, Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network (FANRPAN) Bw. Lufingo Mwamakamba akizungumzia malengo ya warsha wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha Kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Muwasilishaji mada kutoka Taasisi ya CARE International nchini Malawi, Vitumbo Chinoko akiwasilisha mada kuhusu matumizi ya teknolojia katika kusaidia kuhifadhi mazingira wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha Kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Idara ya Menejimenti ya Mazingira Wizara ya Kilimo Bi. Shakwaanande Natai akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa sera ya kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha Kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa nchi kwenye mikutano ya mabadiliko ya tabia nchi kutoka ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Richard Muyungi akizungumzia vionjo vinavyotarajiwa kufanywa kuhusu uhifadhi wa mazingira na kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha Kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Muwasilishaji mada kutoka Taasisi ya CARE International nchini Malawi, Vitumbo Chinoko (wa pili kushoto) akifafanua kanuni za kufauta katika kuhifadhi mazingira na kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi wakati wa mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Idara ya Tafiti zilizoanishwa ESRF, Bi. Vivian Kazi (kulia), Mkurugenzi wa Sera, Mawasiliano na Uragibishi FANRPAN, Francis Hale (wa tatu kulia), Meneja ushirikiano, uragibishi wa sera kutoka taasisi ya Food, Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network (FANRPAN) Bw. Lufingo Mwamakamba (wan ne kulia) pamoja na Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango (kushoto) akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida.
Mkurugenzi wa Sera, Mawasiliano na Uragibishi FANRPAN, Francis Hale akifafanua jambo wakati majadiliano kwenye mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mshiriki akichangia mada wakati wa mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki kwenye mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Sera, Mawasiliano na Uragibishi FANRPAN, Francis Hale (katikati) akibadilishana mawazo na Muwasilishaji mada kutoka Taasisi ya CARE International nchini Malawi, Vitumbo Chinoko (kushoto) wakati wakielekea kwenye eneo la kupiga picha ya pamoja kwenye mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida.
 Picha ya pamoja ya washiriki wa mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
JAMII inayojitambua ndiyo inayoweza kutumika katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha  kushindikana kwa mipango mingi ya udhibiti wa uharibifu wa mazingira kunatokana na uelewa duni na mipangilio isiyozingatia mahitaji halisi ya wananchi wa maeneo husika.
Kauli hiyo imo katika Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ofisi za ESRF.
Katika mdahalo huo uliowezeshwa na Shirika la Kimataifa la Care kwa kushirikiana na taasisi ya FANRPAN na ESRF imeelezwa kuwa kuna changamoto kubwa kwa maendeleo ya kilimo na ukuaji wake kutokana na n chi nyingi Kusini mwa Afrika kutegemea mvua.
Aidha ilielezwa kuwa changamoto nyingine ni umaskini uliokithiri, upungufu nmkubwa wa raslimali watu, maandalizi hafifu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na miundombinu dhaifu.
Mmoja wa watoa mada kutoka Taasisi ya CARE International nchini Malawi, Vitumbo Chinoko alisema kwamba kumekuwa na kulegalega kwa matumizi ya teknolojia katika kusaidia kuhifadhi mazingira miongoni mwa wananchi na uwezeshaji kwa watendaji kiasi cha kuharibu muitikio unaonekana wakati wa mafunzo.
Chinoko alisema kwamba kutokana na hali hiyo walibuni kanuni ambazo wao wanaziita SUPER kanuni ambazo zikifuatwa vyema zinajibu matatizo yaliyopo sasa.
Alisema kwamba Super ni mfumo wa uchakataji wa taarifa na utekelezaji wake unaolenga kuwafikia wananchi wa pembezoni ambao ndio washiriki wakubwa wa utunzaji wa mazingira na uzalishaji wa chakula.
Alisema kwa kutumia kanuni hizo wananchi wanaweza kutambua mwendelezo wa rasilimali ardhi na misitu waliyonayo, wakawezesha kuitumia kwa faida kutokana na uadimu wake.
Aidha kanuni hizo zinahitaji mipango kuzingatia usawa wa kijinsia  ili kuteketeleza sera katika uchumi.
Alisema mfumo wa masoko unazungumzwa ikiwa ni pamoja na ushiriki wa sekta binafsi katika kilimo ili kuipaisha na kuifanya kuwa na tija zaidi.
Alisema kwa sasa kuna tatizo kubwa sana la kuwasilisha taarifa huku watengeneza sera wakiwa pekee yao bila kushirikisha wananchi ambao ndio watendaji wenyewe.
Katika mdahalo huo mada zingine ziliwasilishwa na Bi. Shakwaanande Natai, Mkuu wa Idara ya Menejimenti ya Mazingira Wizara ya Kilimo akishughulikia sera katika kilimo cha kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa nchini Tanzania.
Pia kulikuwa na mada iliyowasilishwa na Bw. Richard Muyungi kutoka ofisi ya Makamu wa Rais ambaye alizungumzia vionjo vilivyokusudiwa katika kuhakikisha wanazungumza kilimo kinachozingatia mabadiliko hali ya tabia nchi (INDCs) Tanzania.
Meneja ushirikiano, uragibishi wa sera kutoka taasisi ya Food, Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network( FANRPAN) Bw. Lufingo Mwamakamba alisema kwamba matokeo ya ushauri  katika mdahalo huo utafikishwa katika kanda na baadae dunia kwa kuwa utekelezaji wa mashauri hayo ni wa lazima kuzingatia mahitaji ya ulinzi wa mazingira kwa kuzingatia kilimo kinachoangalia mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema kwamba watatumia maazimio na ushauri kutoka katika mdahalo huo katika majukwaa mengine muhimu duniani ambayo yanazungumzia makubaliano ya COP 19 na maazimio ya Lome.
Alisema mdahalo huo ni muhimu katika kubaini utayari wa Tanzania na changamoto zake katika kuendesha kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi na kuhakikisha usalama wa chakula na lishe.
Alisema pamoja na kuwepo kwa sera nzuri za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kumekuwepo na hasara kubwa katika kilimo kinachofikia dola za Marekani milioni 200 duniani.
Alisema hasara hiyo ni tishio kwa maisha na kusema kwamba ni vyema wataalamu  naa wananchi wakazungumzia changamoto zilizopo kwa bara la Afrika ambalo linaweza kulisha dunia nzima kama mipango itachambuliwa ipasavyo kwa kushirikisha wananchi na wagani.
Alisema kilimo lazima kifanywe kwa kuzingatia mabadiliko ya hali ya tabia nchi ili kiwe na tija na kukabiliana na mafuriko, ukame, wadudu na magonjwa yanayotokana na mabadiliko hayo.
Bi. Shakwaanande Natai alisema kwamba Tanzania ipo tayari kufanya  kilimo cha kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa kutokana na kuwapo kwa sera na sheria zinazohimiza kilimo chenye tija.
Alisema mipango ya kilimo ya sasa inazingatia mabadiliko hayo pamoja na kutengeneza mfumo wa masoko ili kusaidia watu maskini kabisa wakulima kuwa na uwezo unaotakiwa katika kujisaidia kiuchumi.
Bw. Danford Sango akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida alisema kwamba mdahalo huo ni muhimu kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kuwa tishio kwa ustawi wa wanadamu.
Aidha aliwakaribisha wataalamu kutoka nchi za Kusini mwa Afrika kushiriki katika mdahalo huo wenye tija kwa mataifa ya Kusini mwa Afrika.