Mbunge wa Jimbo la
Kigamboni Mh Dkt Faustine Ndungulile leo
amezindua kituo cha Huduma kwa wateja cha Kampuni ya TUNZAA Digital Holding yenye makao makuu yake
Kigamboni karibu na ofisi za Takukuru mapema leo ijumaa tarehe 08 Julai 2022
akiwa katika kituo hiko amefanikiwa kujionea namna kituo hiko kinavyofanya kazi
na ameweza kuona namna wateja wanavyoweza kununua bidhaa kupitia mfumo wa
TUNZAA ambao unampa nafasi mteja kulipia kidogo kidogo huku mfanyabiashara
akipata taarifa ya manunuzi ya bidhaa yake
Akiwa katika kituo hiko Mh
Ndungulile amesema “Nimefurahishwa sana na ubunifu huu na hakika ni sulushisho
kwa watanzania ambao wanapenda kununua bidhaa kwa kudunduliza na inampa mteja
nafasi ya kutokuwa na deni lakini pia nimefurahishwa na ubunifu kuwa umetoka
katika jimbo langu la Kigamboni na pia nawapongeza wamiliki kwa ubunifu huu
Kituo
hiki cha huduma kwa wateja kitawasaidia wateja na watanzania kuweza kupata
taarifa za namna ya kutumia TUNZAA,
kujiunga TUNZAA kama mnunuzi au muuzaji wa bidhaa au Huduma lakini pia kitatoa
nafasi kwa watanzania ambao hawana simu janja lakini wangependa kununua kwa
kulipa kidogo kidogo ambapo wataweza kutembelea kituo hiko
Mpaka sasa TUNZAA ina watumiaji
Zaidi ya 12,000 huku bidhaa zilizolipiwa mpaka sasa kuwa Zaidi ya 7000 huku
watumiaji wengine wakiendelea kujiunga na mfumo huu ambao unatoa nafuu kwa
wateja kwa kuwapa nafasi ya kulipia bidhaa kidogo kidogo bila kuwa na mawazo
wala madeni
Pia TUNZAA inawakaribisha
wauzaji wa bidhaa mbalimbali ndani ya Tanzania kuweza kujiunga na TUNZAA
kwaajili ya kutanua soko lao kwa watumiaji Zaidi ya 12,000 huku idadi ya
watumiaji ikiendelea kukua kwa kasi sana
TUNZAA imekuwa sulushisho
la maswala ya kifedha kwa kuwasaidia watanzania kuweza kuweka mipango ya
kumiliki au kununua bidhaa zao bila usumbufu wa aina yoyote ule
Ili kuweza kujiunga TUNZAA kama mnunuzi basi uanchotakiwa kufanya
ni kupakua mfumo wetu wa TUNZAA kupitia google playstore na Apple store na
kujiandikisha, na pia Kama wewe ni mfanyabiashara unaweza kujiunga pia kupitia
TUNZAA PLUS inayopatikana katika google store na Apple store
Kwa maelezo Zaidi pia
unaweza kutembelea ofisi zetu zilizopo Kigamboni karibu na ofisi za Takukuru au
kupiga simu 0673 755217 kwa maelezo zaidi
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)