NMB YATUNUKIWA TUZO YA MSHIRIKA BORA MASUALA YA KIFEDHA AFRIKA MWAKA 2018 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

NMB YATUNUKIWA TUZO YA MSHIRIKA BORA MASUALA YA KIFEDHA AFRIKA MWAKA 2018


Kaimu Mkurugenzi wa NMB Bank – Ruth Zaipuna akiwa na tuzo kutoka Shirika la Kimataifa la Fedha ambalo ni tawi la Benki ya Dunia ((IFC) iliyoitaja benki hiyo kuwa Mshirika Bora katika Masuala ya Kifedha kwa nchi za Afrika miongoni mwa benki zinazofanya kazi na shirika hilo.

NMB Bank PLC imeshinda tuzo na kutajwa kuwa Mshirika Bora katika Masuala ya Kifedha Afrika kwa benki zinazofanya kazi na Shirika la Kimataifa la Fedha (IFC) la Benki ya Dunia. Hafla ya kukabidhiwa Tuzo hiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam.

Akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa IFC Afrika Mashariki (IFC Resident for East Africa) Bw. Dan Kasirye, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna alisema "Tumefurahishwa kwa namna ya pekee kupokea tuzo hii ya Kimataifa kutokana na mafanikio yetu; ni ushuhuda wa uwekezaji wetu katika teknolojia huku tukipanua mtandao wa matawi yetu na kuimarisha uwezo wetu wa kutoa huduma nzuri na za kisasa kwa wateja wetu."

Aidha, Bi. Zaipuna aliongeza kuwa “katika miaka minne iliyopita, tumetoa huduma na bidhaa za kisasa na kuendelea kukidhi mahitaji ya wateja wetu nchini kote na kuziba pengo lililoachwa na benki nyingine katika soko. Kwa sasa tuna mtandao mpana zaidi nchini wenye matawi 228, ATM zaidi ya 800 na NMB Wakala zaidi ya 6,000 na hivyo kufanya upatikanaji wa huduma zetu nchini kuwa kwa asilimia 100%”.

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa IFC kwa Afrika Mashariki Bw. Dan Kasirye alisema “NMB Bank imeshinda tuzo hii kutokana na uwezo wake wa kutoa huduma mseto za kifedha zinazomfikia mtumiaji wa chini kabisa. NMB Bank ni mshindi wa ushirikishwaji wa kifedha barani Afrika iking’ara zaidi kuliko benki nyingine zote ambazo zimeshafanya kazi na IFC. NMB imeonyesha uwezo wake katika kuwashirikisha wanawake, biashara ndogo, kubwa na za kati, pamoja na biashara ya kilimo Tanzania.”

TUZO NYINGINE AMBAZO BENKI YA NMB IMESHINDA

Katika kipindi cha miezi 12, Benki ya NMB imeshinda tuzo nyingine mbili za kimataifa ambazo ni; Benki Bora Tanzania kutoka Euromoney Awards for Excellence; Benki Bora ya Wateja Wadogo na Benki Bora ya Biashara Tanzania kutoka Banker East Africa Magazine. Pia benki ya NMB imeshinda tuzo mbalimbali za ndani kama vile; tuzo ya Afya na Usalama Kazini (OSHA) 2018 na tuzo ya utoaji wa taarifa bora za kifedha 2018 kutoka Bodi ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu (NBAA).

Kwa taarifa zaidi wasiliana na:

Joseline Kamuhanda, Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya NMB.

Barua Pepe: Joseline.kamuhanda@nmbtz.com

NMB Bank PLC ni benki inayoongoza Tanzania, kwa idadi ya wateja na hata kwa mtandao wa matawi. Ikiwa na wateja zaidi ya milioni 3, takribani matawi 228 na zaidi ya ATM 800, NMB inawakilishwa katika wilaya zote za Tanzania. NMB inahudumia wateja binafsi, biashara ndogo na za kati, pamoja na biashara kubwa. NMB pia imeandikishwa katika Soko la Hisa la Dar Es Salaam na wanahisa wake wakubwa wakiwa washirika wa kimkakati, Rabobank, wenye asilimia 34.9% ya hisa na Serikali ya Tanzania, yenye asilimia 31.9%.

KUHUSU IFC

International Finance Corporation (IFC) ni taasisi ya kifedha ya kimataifa inayotoa huduma za kiuwekezaji, ushauri, usimamizi wa mali ili kuwezesha maendeleo ya sekta binafsi katika nchi zinazoendelea. IFC ni mjumbe wa World Bank Group na Makao yake Makuu yapo katika Jiji la Washington, nchini Marekani.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages