KANISA Katoliki limetoa msimamo wake juu ya ushiriki wa wanafunzi wa
vyuo vikuu na shule za sekondari katika vyama vya siasa nchini, ikisema
ni hatari na kuwataka wanafunzi hao wazingatie masomo yaliyowapeleka
vyuoni na katika shule hizo.
Msimamo huo umetolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Arusha, Mhashamu Josephat Lebulu katika mahafali ya wahitimu 197 ambao ni madaktari, wauguzi na wataalamu wengine wa afya waliomaliza katika Chuo Kikuu cha Tiba cha KCMC cha Chuo Kikuu cha
Tumaini.
Askofu Lebulu ambaye ni miongoni mwa maaskofu wakongwe wanaoheshimika nchini, alisema wanafunzi hao wanaweza kujifunza masuala ya siasa, lakini si kuwa wanachama wa vyama hivyo na kuungana na wanachama waliopo nje ya vyuo.
“Sina maana ya kupinga kuwapo kwa vyama vya siasa hususani vya upinzani, jambo ninalotaka lieleweke ni kwamba, siasa vyuoni kwa sasa bado wakati wake na hili lisipotazamwa kwa kina huenda tukaendelea kushuhudia migogoro isiyo na kikomo” alisema Askofu Lebulu.
Alisema, kitendo cha wanafunzi hao kujiunga na vyama vya siasa kinaweza kuleta matatizo ndani na nje ya vyuo na shule za sekondari kwa kuwa vijana mara nyingi hutawaliwa na jazba badala ya hoja, hasa wanapokuwa kwenye maandamano.
Askofu Lebulu alisema, hoja za kisiasa, kiuchumi, kitamaduni na kijamii ni nzuri zinapotolewa kisaikolojia, lakini kutawaliwa na jazba ndani ya umma, vyuo au shuleni ni
kuhatarisha amani ya nchi.
Msimamo huo umeungwa mkono na viongozi wa wanafunzi hao, wanafunzi wenyewe na walezi wao na kuitaka Serikali isisitize vyuo vikuu viwe mahali pa kuzalisha wataalamu watakaolitumikia taifa na si mahali pa siasa.
Akiunga mkono kauli ya Askofu, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Wanafunzi Wakatoliki chuoni hapo, Dennis Eavery alisema haoni sababu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kuingiza masuala ya siasa badala ya elimu kulingana na taaluma wanazosomea.
“Mwanya ambao umetolewa na Serikali sanjari na Menejimenti za vyuo unatumiwa vibaya na wanafunzi, hii sasa inasababisha migogoro isiyo na tija kwa vile wanafunzi wanajadili mambo na kuyaweka kisiasa,” alisema.
Kwa upande wake, mwanafunzi Edwiga Francis alisema ipo haja kwa Serikali kuweka utaratibu maalumu kuhusu siasa vyuoni kwani kwa namna moja au nyingine jambo hili limesababisha migogoro baina ya wanafunzi na uongozi wa chuo ikiwemo Serikali kwa ujumla wake.
Akizungumzia kauli ya Askofu Lebulu, Padri Frederick Darksheni alisema siasa imekuwa ikiharibu utaratibu mzima wa masomo kwani wazazi na walezi wamekuwa wakijitahidi kuwagharamia wanafunzi, lakini malengo huwa hayatimii kwani baadhi yao hufukuzwa chuo kutokana na migogoro.
“Siasa siyo mbaya tatizo ni kwamba inazungumzwa na kupewa kipaumbele katika maeneo ambayo bado wakati wake…baadhi ya migogoro vyuoni kwa sasa inachangiwa na mitazamo ya kisiasa,” alisema Padri Darksheni.
Kauli ya Askofu Lebulu imekuja huku kukiwa na mitazamo tofauti katika vyama vya siasa hasa CCM na Chadema kuhusu ushiriki wa wanafunzi hasa wale wa vyuo vikuu katika siasa, kwa baadhi yao kudaiwa kushinikiza migomo na maandamano kwa wanafunzi hao.

CHANZO: HABARI LEO 11 JULY 2011
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)