Wachezaji
wa Yanga ya Dar es Salaam, wakishangilia ushindi na Komne lao baada ya
kukabidhiwa kombe hilo kwa kuibuka kidedea baada ya kuwafunga watani wao
wa jadi Simba kwa bao 1-0, katika mchezo wa fainali ya Kombe la Kagame
uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Bao
hilo lilifungwa na Asamoh baada ya krosi murua kutoka kwa Rashid Gumbo
aliyemtoka Ulimboka mwakingwe katika dakika za nyongeza baada ya
kumalizika dakika 90 bila kufungana.
Ubao ulisomeka hivi hadi mwisho wa mchezo huo.
Kipa
wa Simba Juma Kaseja, akiruka kuokoa mpira bila mafanikio uliopigwa na
Asamoh kwa kichwa na kuandika bao la kwanza na la ushindi kwa Yanga.
Liziwani Kikwete (kulia) akishangilia ushindi wa Yanga na shabiki mwenzake, Muddy Sebene, baada ya mchezo huo kumalizika.
Hekaheka langoni mwa Simba.
Na Sufiani Mafoto
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)