Mtangazaji
na Modo Jestina akionyesha mitindo ya mavazi kutoka kwa mbunifu Anna
Lukindo na pichani juu ni mamodo wa Anna katika pozi
Mama Balozi na staff wa Ubalozi nao walitokea kumsupport Mtanzania mwenzao
Kutoka kushoto: Marium Kilumanga, Jestina George, Anna Shelukindo na mdau wakila pozi
SALAM,
Mtanzania
mbunifu wa mitindo ya nguo, Anna Lukindo, ametikisa ulimwengu wa
fashion jijini london wikiendi iliopita. Anna alionyesha mavazi
aliyobuni kwenye maonyesho ya La Geneve North Event, yaliyofanyika
London siku ya Ijumaa tarehe 8.7.11 Ubunifu wa Anna ulipokelewa kwa
vifijo na nderemo kwani ulikuwa ndio uliotia fora.
Kulikuwa
na wabunifu wengine kumi, lakini Anna ndiye alikuwa mwafrika na
Mtanzania pekee ambaye mavazi yake yalikubalika na kupendwa na watu
wengi zaidi.
Mojawapo
ya wageni na wadau mbalimbali walijjitokeza kumpa sapoti Anna ni Mh.
Balozi wetu Peter Kallaghe na Mama Balozi, Naibu Balozi Chabaka
Kilumanga pamoja na watanzania wengine.
Kwa niaba ya URBAN PULSE, tunapenda Kumpongeza Dada yetu Anna Na Kumtakia kila la kheri pamoja na Mafaniko Mema.
Kwa mawasiliano zaidi na Anna tembelea
Kwa mawasiliano zaidi na Anna tembelea
Pr/Media:Pauladpope@yahoo.co.uk
Web:www.annaluks.com
Twitter:@AnnaLukindo
imeletwa kwenu na:
URBAN PULSE CREATIVE
Urbanpulsecreative@googlemail.com
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)