Mkurugenzi wa Maji Mijini wa Wizara ya Maji, Mary Mbowe (kulia), akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima cha maji cha Mzinga A, kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika eneo la Kitunda Nyangasa, Dar es Salaam jana.Kutoka kushoto ni Mhandisi Ujenzi wa TBL, John Malisa, Mwenyekiti wa mradi huo, Rashid Nandonde na Meneja Miradi Maalumu wa TBL, Emma Orio. Mkazi wa Kitunda Nyangasa, Dar es Salaam, Pili Khamis, akifurahi kupata maji baada ya Mkurugenzi wa Maji Mijini wa Wizara ya Maji, Mary Mbowe (kulia) kuzindua kisima cha maji cha Mzinga A, kilichojengwa kwa sh. milioni 27 zilizotolewa msaada na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)