Dr Willibrod Slaa
Duru za siasa nchini Tanzania zinasema baada ya Chama cha Mapinduzi kuwataka wanaojijua mafisadi ndani ya chama hicho kujiondoa na kujivua gamba ndani ya siku 90, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, leo ataweka hadharani orodha ya pili ya majina ya watuhumiwa mafisadi baada ya ile ya awali aliyoitoa mwaka 2007, Mwembeyanga.
Septemba 15, 2007, Dk. Slaa akiwa wilaya ya Temeke katika viwanja vya Mwembeyanga aliwataja vigogo 11 wanaodaiwa kuwa ni mafisadi akiwemo aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Nchini (BOT) ambaye sasa ni marehemu Dk. Daudi Balali, Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge, na Basil Mramba aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Rombo.
Wengine ni Gray Mgonja aliyekuwa Katibu Mkuu mstaafu, Hazina; Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Patrick Rutabanzibwa; Kada wa Nazir Karamagi; mbunge wa Musoma Vijijini Nimrod Mkono ; mbunge wa Igunga Rostam Aziz ; mbunge wa Monduli Edward Lowassa ; Rais mstaafu wa Awamu ya ....,na....
Dk. Slaa ambaye yupo mkoani Tabora akiongozana na viongozi wengine katika ziara ya kukijenga chama mkoani humo atafanya mkutano wa hadhara na kutaja orodha hiyo mpya baada ya CCM kushindwa kutaja majina ya mafisadi hao.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)