Mashabiki wa Mada Maugo wakimbeba juu juu Mada huku wakishangilia ushindi, baada ya kumalizika kwa pambano hilo na kutangazwa mshindi.
Bondia Yohana Robert (kulia) akimchakaza mpinzani wake Said Zungu, wakati wa pambano lao la utangulizi la raundi 10 la kuwania ubingwa wa TPBO, ambapo Yohana alishinda pambano hilo katika raundi ya nne baada ya Zungu kutokwa na damu nyingi usoni jambo lililomfanya kutoendelea na pambano hilo Yohana kutwaa mkanda.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, David Misime, akimvisha mkanda Yohana Robert baada ya kuibuka mshindi katika pambano lake la kuwania ubingwa wa TPBO na mpinzani wake, Said Zungu.
Mohamed Matumla (kulia) akichuana na mpinzani wake, Sadiq Momba, bondia mwenye makeke awapo jukwaani kama anavyoonekana akikwepa konde kwa staili ya aina yake huku mguu mmoja akiwa ametinga kiati na mguu mmoja Soksi, hii ilitokea wakati alipokuwa akijaribu kubadilisha viatu kutokana kuteleza mara kadhaa, kwa bahati mbaya muda wa mapumziko ukamalizika na kumlazimu kurejea ulingoni bila kiatu kimoja.
Bondia Japhet Kaseba (kushoto) akichuana na Mada maugo wakati wa pambano lao lisilo la ubingwa la raundi nane lililofanyika kwenye Ukumbi wa PTA Sabasaba Temeke Dar es Salaam jana. Pambano hilo lilimalizika katika raundi ya saba baada ya mabondia hao kuchezeana faulo bila mwamuzi kusimamisha mchezo na Kaseba kuamua kuvua glovz kugoma kuendelea na pambano na Maugo kutangazwa mshindi.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)