Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Said Mwema, amewatoa machozi wananchi kufuatia ujumbe wake mfupi wa maneno kwa njia ya simu (SMS) iliyokuwa ikilalamikia kitendo cha baadhi ya wanakijiji wa Mwakashahala kumuua polisi Joseph Milinga aliyewakamata wakiwa na bangi.
IGP Mwema alikuwa akiwalalamikia watu hao kwa vile kitendo alichokuwa akikifanya marehemu kilikuwa cha kuzuia mihadarati hiyo isisambae na kuharibu watoto au kizazi kijacho.
Aidha, katika meseji hiyo iliyonaswa na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita, pia Mwema alionesha kukerwa na tabia iliyoota mizizi ya watu kujichukulia sheria mikononi. Akahoji, wako wapi watu wema?
Maelezo kamili ya meseji hiyo yanasomeka kama ifuatavyo:
Salam, nakutakia heri ya Pasaka. Pia naomba tafakari mob justice (kujichukulia sheria mikononi) ni adui wa human rights rule of law,(sheria za haki za binadamu).
Good governance (Utawala bora) iwe kwa raia au askari aliyeuawa Tbr (Tabora) ambaye niko njiani kwenda Rukwa kumzika.
Na iwe sababu yoyote, hata Mungu hampendi anayetoa kikatili roho ya mtu mwingine na hasa anapotaka kukamata bangi ili isidhuru watoto wetu na watu wengine.
Where are the good people? (Wako wapi watu wema?) Lets join hands and have ant mob justice campaign in this country for common good

(Tushikamane kupinga wanaojichukulia sheria mikononi katika nchi kwa ajili ya ustawi).
Baadhi ya watu waliokutwa wakiisoma meseji hii walionesha kusikitishwa sana na tabia ya watu kujitwalia sheria mikononi wakati vyombo vya sheria vipo na wengine walishindwa kujizuia kutokwa machozi.
Afande Milinga, aliuawa na wananchi waliojiita wenye hasira kali wakati akitimiza wajibu wake wa kazi akiwa katika zoezi la kusaka watu wanaolima na kuuza Bangi.
Tukio hilo lilitokea Aprili 20, mwaka huu katika kijiji cha Mwakashahala, kata ya Puge, wilayani Nzega, Mkoa wa Tabora.
Wananchi hao walimshambulia marehemu kwa silaha mbalimbali za jadi mpaka kifo chake.
Mbali na marehemu, afande mwingine aliyekuwa naye alijeruhiwa vibaya na kulazwa hospitali ya Mkoa wa Tabora.
Mbali na tukio hilo, vitendo vya raia kuua askari katika kijiji hicho hii ni mara ya pili.
Marehemu Milinga alizikwa katika kijiji cha Kisiwa cha Manda Karenge, kata ya Kirambo, wilayani Nkasi, Mkoa wa Rukwa, ameacha mke na watoto wanne.
Wakati huo huo, IGP Mwema amewataka wananchi wa Kijiji cha Mwakashahala waliokimbia makazi yao wakihofia kukamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za mauaji, warudi na kuungana na familia zao kwani watuhumiwa wameshakamatwa na wanahojiwa na jeshi lake.
Akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo Jumamosi iliyopita, Kamanda Mwema alisema hakuna haja ya mtu kukimbia kama hakuua, kwa sababu jeshi lake halimkamati kila mtu.
Katika kipindi hiki cha uongozi wake, IGP Mwema amefanikiwa kuifanya jamii iliamini jeshi la polisi tofauti na miaka ya nyuma.
Aidha, hali ya utulivu imeongezeka, sanjari na kupungua kwa ujambazi ambao zamani ulikuwa ukitikisa nchi.

Kwa Msaada Wa Global Publishers Tanzania
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)