Taarifa Zilizotufikia hivi punde Maeneo ya Segerea Stand Ya Mabasi Kipande cha bomu kimedondokea hapo ila hakuna mtu aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha na Eneo hilohilo la Segerea Ilipo Sheli ya Mafuta Kipande cha Bomu kimedondoka na kuchimba na Wanajeshi Wamefika Eneo Hilo la Tukio Kwa ajili ya usalama.
Maeneo ya Ilala Tumepata habari kuwa watoto ambao idadi yao haikuweza kujulikana wamepoteza maisha baada ya kukanyagwa wakati wakikimbia na wengine kugongwa na Magari.
Maeneo Ya Kambi Ya Jeshi Ni kwamba kuna nyumba moja ambayo ipo karibu na kambi hiyo ya jeshi imeungua baada ya kuangukiwa na vipande vya mabomu na wakati huo huo nyumba nyingine sehemu hiyohiyo ikiendelea kuungua baada ya kuangukiwa na vipande vya mabomu. Hadi hivi sasa Chanzo cha kulipuka kwa mabomu hayo bado hakijajulikana na Ulinzi umeimarishwa na wananchi wanaombwa kutofika kabisa katika maeneo hayo na sehemu ya mwisho wa wananchi kufika ni Airport.
Milipuko ya mabomu yametokea katika ghala namba tano (5) ya jeshi la wananchi la Tanzania kambi ya Gongo la mboto. Endelea Kuwa Na LJ BLOG kwa taarifa zaidi punde zitakapotufikia kutoka kwa ripota wa LJ BLOG.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)