Mabomu yalipuka katika Kambi ya Jeshi la Wananchi Wa Tanzania iliyopo Maeneo Ya Gongo La Mboto, wakazi waishio karibu na eneo la tukio wakimbia ovyo huku wengine wakikimbia wasipojulikana.Jeshi la Polisi limewaombaWakazi hao kukaa ndani na kufunga milango na wasikimbilie eneo ambalo mabomu yanalipuka.Mabomu hayo yameanza kulipuka mida ya saa tatu usiku huu. Na Hali katika Jiji la Dar hali ni tete kutokana na Milipuko YA mabomu hayo na Taarifa iliyotufikia punde hapa Wakazi Wengi Waliopo karibu na Kambi hiyo na maeneo jirani wakimbia ovyo na idadi yao ni kubwa na barabara hazipitiki kutokana na idadi kubwa ya watu kukimbia ovyo barabara na Network za Simu Zinasumbua.Chanzo Cha Milipuko hiyo hadi Sasa hakijaulikana na Waziri Wa Ulinzi Mh Mwinyi Amesema Atoa Taarifa Kuhusu Milipuko Hiyo ambayo inaendelea kulipuka.Tutazidi Kuwataarifu kadri taarifa zitakavyotufikia kutoka kwa ripota wa LJ BLOG kwa hiyo tuwe na subira.
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)