
Mkuu
wa kitengo cha elimu kwa Umma kitengo cha Usalama barabarani makao
makuu ya Polisi ASP,Abel Swai(kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Maofisa wa
Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro pamoja
na Ofisa wa Vodacom Tanzania, Heladius Kisiwani(katikati) kabla ya
kuanza zoezi la kutoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi
wakati wote wakitumia vyombo vya moto ikiwa ni mwendelezo wa kampeni
ya”Wait to Send”inayoendeshwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na
Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani,ilifanyika jana katika
Stendi kuu ya mabasi ya Msamvu mkoani Morogoro.

Abiria
wa Mabasi yaendayo mikoani wakimsikiliza Mkuu wa kitengo cha elimu kwa
Umma kitengo cha Usalama barabarani makao makuu ya Polisi ASP,Abel
Swai,wakati alipokuwa anawalelimisha abiria hao ndani ya basi
linalofanya safari zake mikoani ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni
ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi
wakati wote wakitumia vyombo vya moto.Kampeni hiyo inaendeshwa na
Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo hicho
ilifanyika jana katika Stendi kuu ya Msamvu mkoani Morogoro.

Maofisa
wa Jeshi la Polisi Usalama Barabarani Mkoani Morogoro,wakimsikiliza
Kaimu mkuu wa kanda ya kati wa Vodacom Tanzania,Heladius
Kisiwani(kulia)wakati alipokuwa akiwapa maofisa hao maelezo kuhusiana na
pete ya kidoleni inayotolewa na Kampuni hiyo kwa kushirikiana na jeshi
hilo yenye ujumbe“Wait To Send” unaohamasisha madereva wa vyombo vya
moto kutokutumia simu za mkononi wakiwa wanaendesha vyombo hivyo,Zoezi
hili lilifanyika jana katika kituo cha mabasi yaendayo mkoani cha Msamvu
mkoani Morogoro.

Askari
wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Morogoro,SGT.
John Masawe(kushoto)akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la
kwenda mikoani,Rajabu Abdallah ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya”Wait
to Send”inayoendeshwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la
Polisi kitengo hicho.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)