Pages

JESHI LA POLISI KITENGO CHA USALAMA BARABARANI PAMOJA NA VODACOM TANZANIA WAENDELEA KUTOA ELIMU KWA MADEREVA NA ABIRIA KUPAZA SAUTI

Mkuu wa kitengo cha elimu kwa Umma kitengo cha Usalama barabarani makao makuu ya Polisi ASP,Abel Swai(kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Maofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro pamoja na Ofisa wa Vodacom Tanzania, Heladius Kisiwani(katikati) kabla ya kuanza zoezi la kutoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayoendeshwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani,ilifanyika jana katika Stendi kuu ya mabasi ya Msamvu mkoani Morogoro.

Abiria wa Mabasi yaendayo mikoani wakimsikiliza Mkuu wa kitengo cha elimu kwa Umma kitengo cha Usalama barabarani makao makuu ya Polisi ASP,Abel Swai,wakati alipokuwa anawalelimisha abiria hao ndani ya basi linalofanya safari zake mikoani ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto.Kampeni hiyo inaendeshwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo hicho ilifanyika jana katika Stendi kuu ya Msamvu mkoani Morogoro.
Maofisa wa Jeshi la Polisi Usalama Barabarani Mkoani Morogoro,wakimsikiliza Kaimu mkuu wa kanda ya kati wa Vodacom Tanzania,Heladius Kisiwani(kulia)wakati alipokuwa akiwapa maofisa hao maelezo kuhusiana na pete ya kidoleni inayotolewa na Kampuni hiyo kwa kushirikiana na jeshi hilo yenye ujumbe“Wait To Send” unaohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakiwa wanaendesha vyombo hivyo,Zoezi hili lilifanyika jana katika kituo cha mabasi yaendayo mkoani cha Msamvu mkoani Morogoro.
Askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Morogoro,SGT. John Masawe(kushoto)akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la kwenda mikoani,Rajabu Abdallah ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayoendeshwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo hicho.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)