SHIRIKA
la ndege la Etihad ambalo ndio shirika rasmi la nchi ya Falme za
kiarabu, leo hii limetangaza makubaliano na kampuni ya Luggage Logistics
kuboresha mfumo mzima wa usimamizi wa mizigo katika viwanja vake vya
ndege dunia nzima.
Kupitia
mfumo wa kisasa wa Baggage Management System (BMS) unaosimamiwa na
kampuni ya Luggage Logistics, shirika la ndege la Etihad litaweza
kuboresha usimamizi ikiwemo kusafirisha mizigo ya wasafiri kwa wakati.
Mfumo huo pia utawezesha kufuatilia kwa urahisi mizigo iliypotea njiani
dunia nzima.
Mfumo
wa BMS utahusisha ratiba za ndege, taarifa za wasafiri pamoja na mifumo
ya udihibiti safari zote ka pamoja. Hii itasaidia kuongeza kasi
taratibu za kutambua mizigo ya abiria na kisha kuhamisha mizigo toka
kwenye ndege hadi uwanja wa ndege na hatimaye kwenda kwenye ndege ya
kuunganisha safari husika, ikisaidia safari kutochelewa.
Mfumo
huu umeunganishwa katika kituo kimoja cha udhibiti ambapo taarifa zote
za mizigo kutoka vyanzo mbalimbali hutunzwa. Taarifa hizi zinaweza
kusambazwa haraka na uwepesi baina ya vitengo husika dunia nzima.
Geert
W. Boven, Makamu rais wa Huduma za viwanja vya ndege kutoka Etihad,
alisema: “Ushirikiano na kampuni ya Luggage Logistics kutaongeza ufanisi
zaidi katika kutambua, kusimamia na kusafirisha mizigo ya abiria
duniani kote kwenye viwanja vyetu tukianzia na hapa Abu Dhabi.
Mfumo
mpya huu utasaidia kuboresha huduma kwa abiria kwa kupunguza upotevu wa
mizigo, kupunguza idadi ya safari zinazochelewa juu ya kupotea kwa
mizigo pamoja na kuongeza ufanisi wa huduma zetu za uwanja wa ndege”
Adam
Dalby, Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Luggage Logistics, alisema
“Tunayofuraha kushirikiana na shirika la ndege la Etihad, shirika ambalo
tupo pamoja katika kutambua umuhimu wa uvumbuzi na huduma bora. Kupitia
mfumo huu wa kisasa wa BMS, taarifa za papo hapo hupatikana na hutumika
kuhakikisha mizigo ya abiria inasimamiwa kwa ufanisi zaidi safari
nzima”
Shirika
la ndege la Etihad lilichagua mfumo wa BMS kwani unakidhi mahitaji na
vigezo vyote vya usimamizi mizigo, ikiwemo ICAO Annex 17 pamoja na
maazimio ya IATA, mfumo huu unaweza kuunganishwa na mitambo ya shirika
hili la ndege bila ugumu wowote pia. Suluhisho hili limewiana na
uendeshaji na mahitaji ya miundombinu ya Shirika la ndege nay ale ya
kituo cha Abu Dhabi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)