Redd’S Miss Arusha City Centre 2013, Nancy Moshi
akipunga mkono mara baada ya kutawazwa mshindi wa Taji hilo katika shindano
lililofanyika Usiku wa kuamkia jana jijini Arusha. Nancy aliwashinda warembo
wenzake 10 waliokuwa wakiwania nae taji hilo.
Redd’S Miss Arusha City Centre 2013, Nancy Moshi
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Glory Steven
(kushoto) na mshindi wa tatu Neema Kessy mara baada ya warembo hao kutangazwa
kuwa ndio washindi wa shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia jana jijini
Arusha.
Warembo wanaliokuwa wakiwania taji la Redd’s Miss
Arusha City Centre 2013 wakicheza show ya ufunguzi wa shindano hilo jijini
Arusha usiku wa Kuamkia leo.
Wadau mbalimbali wa sanaa ya Urembo mjini Arusha wakifuatilia Onesho hilo la Redd's Miss Arusha 2013.
Mwandaaji wa shindano hilo Bi Upendo (kulia) na rafiki yake.
Warembo walimfanyia tukio la kipekee Mwandaaji wao kwa Keki ya Birthday, na hapa Upendo akizima mishumaa hiyo...
Warembo wa tano kati ya 11 waliokuwa wanawania taji la
Redd’s Miss Arusha City Centre 2013 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
kutangwaza kufuzu hatua hiyo. Kutoka kushoto ni Minael Anderson, Neema Joel,
Nancy Moshi, Neema Kessy na Glory Steven.
Mwana dada Rachel ndiye aliyekuwa msanii kinara wa show hiyo na hapa akicheza na mashabiki wake.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)