Baadhi ya wakazi wa eneo la wazi lililovamiwa na
kumilikiwa isivyo halali na watu maeneo ya Madale, Kinondoni Dar es Salaam,
ambako Polisi walikuwa wakiendesha oparesheni ya kuvunja nyumba na vibanda vyao,
wakiwa wamewekwa kwenye gari tayari kupelekwa kituo cha Polisi cha Oysterbay
jijini.
Askari
Polisi akiangalia mabaki ya kibanda kilichobomolewa na tingatinga la Manispaa ya
kinondoni wakati wa zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la
wazi maeneo ya Madale, Kinondoni jijini Dar es Salaam juzi.
Askari Polisi akiangalia badhi ya vifaa vilivyokuwemo
ndani ya moja ya kibanda kilichobomolewa na tingatinga la Manispaa ya Kinondoni,
wakati wa zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi maeneo
ya Madale, Kinondoni jijini Dar es Salaam juzi.
Askari Polisi wakiangalia mabaki ya kibanda
kilichobomolewa na tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, wakati walipokuwa
wakisimamia zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi
maeneo ya Madale, Kinondoni jijini Dar es Salaam juzi.
Askari
Polisi, akimuongoza mmoja wa vijana
waliokuwa wakiwatishia, wakati walipokuwa wakisimamia zoezi la kuvunja nyumba na
vibanda vya wavamizi maeneo ya wazi, Madale Kinondoni, jijini Dar es Salaam
kuelekea kwenye gari tayari kwa kuwapeleka kituoni juzi.
Mmoja wa
askari Polisi, akimuongoza kijana mwingine aliyekuwa
akiwatishia, wakati walipokuwa wakisimamia zoezi la kuvunja nyumba na vibanda
vya wavamizi maeneo ya wazi, Madale Kinondoni, jijini Dar es Salaam kuelekea
kwenye gari tayari kwa kuwapeleka kituoni juzi.
Askari
Polisi wakiwa wamesimama sehemu kilipobomolewa moja ya vibanda juzi,
vilivyojengwa kwenye sehemu za wazi zinazodaiwa kuvamiwa isivyo halali na watu
ambao walikuwa wakiviuza kwa baadhi ya wananchi maeneo ya Madale, Kinondoni, Dar
es Salaam.
Tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, likivunja moja ya
vibanda vilivyojengwa kwenye eneo lililovamiwa maeneo ya Madale Kinondoni jijini
Dar es Salaam juzi.
Dereva wa
gari la Jambo Leo, Privatus Kachema, akiangalia zoezi la uvunjaji wa nyumba na
vibanda vya wavamizi maeneo ya Madale Kinondoni, jijini Dar es Salaam juzi.
Moja ya
nyumba zilizovunjwa katika oparesheni ya uvunjaji wa nyumba na vibanda vya
wavamizi wa eneo la wazi la Madale juzi.
Tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, likivunja moja ya
vibanda vilivyojengwa kwenye eneo hilo la wazi.
Tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, likiendelea kuvunja
moja ya vibanda vilivyojengwa kwenye eneo.
Askari Polisi na Mgambo wa Manispaa ya Kinondoni,
wakikagua moja ya kibanda kabla ya kuvunjwa na tingatinga la Manispaa hiyo,
wakati wa zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi Madale
Kinondoni, jijini Dar es Salaam juzi.
Askari
Polisi na mgambo wa Manispaa ya Kinondoni wakiangalia tingatinga la Manispaa
hiyo, wakati likivunja nyumba na vibanda vilivyojengwa kwenye sehemu za wazi
zinazodaiwa kuvamiwa isivyo halali na watu ambao walikuwa wakiviuza kwa baadhi
ya wananchi wengine maeneo ya Madale wilayani
humo.
Askari Polisi wakiangalia mabaki ya kibanda
kilichobomolewa na tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, wakati walipokuwa
wakisimamia zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi
maeneo ya Madale, Kinondoni jijini Dar es Salaam juzi.
Moja ya
bango lililokutwa limeandikwa na watu hao, likiwa na ujumbe uliokuwa ukimshutumu
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela na OCD
wake.
Mmoja wa
watu wanaodaiwa kuwa wavamizi wa eneo hilo, aliyejitambulisha kwa jina la
Hussein Said, akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kupata athari kichwani wakati
alipokuwa akiwekwa chini ya ulinzi na askari Polisi kwenye maeneo hayo. Picha zote na Kassim Mbarouk wa Bayana Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)