KIJANA APOTEZA MAISHA PAPO HAPO MARA BAADA YA KUKANYAGWA NA LORI NA KUPELEKEA KICHWA KUPASUKA NA UBONGO KUTOKA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KIJANA APOTEZA MAISHA PAPO HAPO MARA BAADA YA KUKANYAGWA NA LORI NA KUPELEKEA KICHWA KUPASUKA NA UBONGO KUTOKA

 Baadhi ya wananchi wakiwa wanaangalia mwili wa marehemu ambaye amepoteza maisha papo hapo mara baada ya kugongwa na lori na kukanyagwa kichwa na hatimaye kupelekea kichwa kupasuka na ubongo kumwagika chini leo majira ya saa tisa mchana eneo la ilala boma
 Mwili wa marehemu  ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja ukiwa umefunikwa na kanga huku pembeni vipande vya ubongo wake vikiwa pembeni mara baada ya kugongwa na lori na kukanyangwa kichwa na kupelekea kichwa kupasuka na ubongo wote kumwagika chini leo majira ya saa tisa mchana eneo la Ilala Boma. Kijana huyu anasadikiwa kuwa ni mwanafunzi wa Darasa la Saba katika shule ya Msingi Msimbazi.
 Askari wa Usalama barabarani akisaidiana na baadhi ya wananchi kuubeba mwili wa marehemu ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja ili kuupakia katika gari dogo tayari kuupeleka hospitali ya Amana.Kijana huyu anakadiriwa kuwa ni mwanafunzi wa Darasa la Saba wa Shule ya Msingi Msimbazi.
 Baadhi ya wananchi wakiutazama mwili wa marehemu ambaye amegongwa na gari na kupelekea kupasuka kichwa na kupoteza maisha papo hapo.
Mwili wa marehemu ukifunikwa vizuri kwaajili ya kupelekwa hospitali ya amana.Pembeni ya mwili wa marehemu ni vipande vya ubongo mara baada ya kukanyangwa na lori

Na Josephat Lukaza - Lukaza Blog 

Kijana wa kiume ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja amepoteza maisha mara baada ya kugongwa na lori leo majira ya Saa tisa Mchana eneo la Ilala Boma karibia na Ofisi ya Mkuu Wa Mkoa wa Dar Es salaam. Mara baada ya kugongwa na lori, lori hilo liliweza kukimbia na halikujulikana ni wapi limeelekea na namba za gari hizo hazikuweza kupatikana mara moja.

Kijana huyu anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 14 ambaye pia shuhuda wa ajali hii ameueleza mtandao wa lukaza blog kuwa ni mwanafunzi wa shule ya msingi Msimbazi Center kutokana na sare za shule alizokuwa amevaa.

Shuhuda wa Ajali hii ambaye hakupenda jina lake kuchorwa na mtandao wa LUKAZA amesema kuwa Wakati kijana huyo anavuka barabara lori lililomgonga lilikuwa linatokea maeneo ya buguruni na kumgonga kijana huyo. Mara baada ya kumgonga lilimkanyaga kichwani " Lilianza tairi la mbele kumkanyaga kichwa halafu likafuatia na tairi la nyuma ambapo lilipelekea kichwa kupasuka vibaya na hatimaye ubongo kusambaa barabarani kama ambavyo unao hapo chini na hatimaye lori hilo kukimbia" alisema shuhuda huyo.

LUKAZA BLOG ilimuuliza shuhuda huyo kwanini akunakili namba za usajili wa lori hilo

na hivi ndivyo shuhuda wetu alivyojibu " Kiukweli Nilishindwa kuandika au kunakili namba ya usajili wa lori kwasababu kwanza niliposikia kitu kizito kimegongwa na hilo lori nilijua ni mtu wa bodaboda wakati naangalia vizuri nikaona ni kijana mdogo ndiye amegongwa na lori likimkanyaga kichwa likiwa katika harakati ya kukimbia hapo nilishindwa kuandika chochote kwasababu nilipigwa na butwaa na kubaki kama bumbuwazi na mwili kushikwa na ganzi mara baada ya kuona ubongo vipande vya ubongo chini" alisema shuhuda wetu

Mpaka mtandao wa lukaza blog unaondoka eneo la tukio lori lililomgonga halikuweza kupatikana wala kujulikana lilipoelekea na jina la kijana aliyepoteza uhai papo hapo nalo halikuweza kupatikana 

Lukaza blog Inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki waliompoteza ndugu yao

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZO JUU

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEPA PEPONI AMINA

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages