Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa kufuata Sheria za Kiislamu wa Benki ya NBC, Yassir Masoud (katikati) akionyesha kadi ya ATM ya akaunti ya kiislamu ya benki hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ambayo wateja wawili wa akaunti hiyo watajishindi tiketi mbili kila mmoja zitakawawezesha kusafiri kwenda kuhiji Makka mwezi Oktoba. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Mussa Kundecha na kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Suleiman Lolila.
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) leo
imezindua kampeni ya miezi miwili kwa ajili ya wateja wake wa huduma za
kibenki zinazofuata sheria za kiislamu, ili kubaini washindi
watakaoshinda Safari ya wawili iliyolipiwa kila kitu kwenda kuhiji Makka
mwezi Oktoba 2012.
Kampeni
hiyo ambayo ilizinduliwa katika Ofisi za Makao Makuu ya NBC ni sehemu
ya sherehe za miaka 45 za benki ya NBC kutoa huduma za kibenki. Sherehe
hizi zitawezesha wateja kushinda zawadi mbalimbali zilizotayarishwa kwa
ajili yao.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Idara ya kutoa huduma za kibenki kwa
kufuata Sheria za Kiislamu wa NBC, Yassir Masoud alisema,"Kampeni hii
siyo tu kwa ajili ya kusherehekea miaka 45 ya kutoa huduma bora za benki
kwa wateja wetu lakini pia kusherehekea miaka miwili ya kutoa Huduma za
kibenki zenye kufuata sheria za Kiislamu".
"Hii
ni mara ya kwanza kwa kampeni ya aina hii kufanyika nchini na
tunawakaribisha wateja wetu wote na yeyote mwenye nia ya kushiriki,
washiriki kikamilifu ili kupata nafasi ya kushinda zawadi hii ya
kipekee" alisema Bwana Masoud.
NBC
ilianza kutoa huduma za benki zinazofuata Sheria za Kiislamu tangu
mwezi Mei 2010. Hivi sasa huduma inayotolewa ni pamoja na Akaunti za
Akiba za Kiislamu na Akaunti za Hundi. Hivi karibuni pia benki ilizindua
ya Akaunti za Biashara za Kiislamu na akaunti za Kiislamu kwa
Mashirika. Huduma hizo zinatolewa bila riba, na kwa kufuata Sheria za
Kiislamu, pia ni wazi kwa wateja wote bila kujali imani zao.
Kampeni
iliyozinduliwa leo itaisha Septemba 13, 2012, ambapo washindi
watachaguliwa kwa njia ya droo. Washindi watajishindia safari
iliyolipiwa kila kitu kwa ajili ya watu wawili kwenda Kuhiji. Zawadi ni
pamoja na tiketi za ndege, malazi na fedha za matumizi wakati wa safari
hiyo ya kwenda Makkah.
Kwa Wahariri; NBC
ni kampuni ya kutoa huduma za kifedha inayojali wateja. Tunashirikiana
na wadau wetu wote ili kujenga mafanikio kwa mbinu zinazotizama maslahi
ya mteja, ubunifu na utofauti wa bidhaa
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Mussa Kundecha (kushoto)
akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampuni ambayo wateja wawili wa
akaunti ya kiislamu ya NBC watajishindia tiketi mbili kila mmoja
zitakazowawezesha kusafiri kwenda kuhiji Makka kwa gharama za NBC Mwezi
Oktoba. Uzinduzi ulifanyika jijini Dar es Salaam
leo. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa kufuata Sheria
za Kiislamu wa Benki ya NBC, Yassir Masoud na kulia ni Katibu Mkuu wa
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Suleiman Lolila.
Daima Karibu Nawe
Kwa Taarifa Zaidi Wasiliana na;
Mshauri wa Mahusiano ya Umma wa NBC, Eddie Mhina, eddie.mhina@nbctz.com
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)