Rais Jakaya Mrisho
kikwete, Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda na mkewe Mama Janet
Museveni, Waziri Mdogo wa Uingereza wa Maendeleo ya Kimataifa Bw.
Stephen O'Brien (kulia) na Mama Melinda Gates wakibadilishana mawazo
kabla ya kuhutubia katika mkutano wa kimataifa wa viongozi kujadili Uzazi
wa Mpango kwa nchi masikini zaidi duniani katika ukumbi wa Queen Elizabeth II jijini London July 11, 2012. Mkutano huo ni
wa kwanza wa aina yake duniani na umeanzisha Mchakato wa Dunia ambao utalenga
kuwawezesha wanawake wapatao milioni 120 katika nchi masikini zaidi duniani
kupata habari, huduma na mahitaji ya kupanga uzazi bora zaidi na kuokoa maisha
yao ifikapo mwaka 2020.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akuhutubia katika mkutano wa kimataifa wa viongozi kujadili Uzazi
wa Mpango kwa nchi masikini zaidi duniani, katika ukumbi wa Queen Elizabeth II jijini London July 11, 2012. Mkutano huo ni
wa kwanza wa aina yake duniani na umeanzisha Mchakato wa Dunia ambao
utalenga kuwawezesha wanawake wapatao milioni 120 katika nchi masikini
zaidi duniani kupata habari, huduma na mahitaji ya kupanga uzazi bora
zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. Donald Cameron, Rais Paul
Kagame wa Rwanda na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakijiandaa
kupanda jukwaani kuhutubia katika mkutano wa kimataifa wa viongozi kujadili Uzazi
wa Mpango kwa nchi masikini zaidi duniani. katika ukumbi wa Queen Elizabeth II jijini London July 11, 2012. Mkutano huo ni
wa kwanza wa aina yake duniani na umeanzisha Mchakato wa Dunia ambao
utalenga kuwawezesha wanawake wapatao milioni 120 katika nchi masikini
zaidi duniani kupata habari, huduma na mahitaji ya kupanga uzazi bora
zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa British Gas (BG Group), Sir Frank
Chapman alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo mjini Reading
Uingereza Julai 11, 2012. BG Group imewekeza kiasi cha Pauni 80 za
Uingereza (Shilingi Trilioni 125) katika mradi wa kuchimba gesi asilia
nchini Tanzania, na tayari visima vitano vya nishati hiyo vimeshatema
gesi nyingi katika bahari kuu kusini mwa Tanzania maeneo ya Mtwara. Hii
ilikuwa ni ziara fupi katika makao makuu ya BG Group mjini Reading,
Uingereza ambako Rais Kikwete na ujumbe wake walitembelea Julai 11
kujionea namna kazi za uvumbuzi wa gesi asilia unavyofanywa na kampuni
hiyo yenye kufanya shughuli zake katika nchi 21 katika mabara matano,
ikiwa na jumla ya wafanyakazi 6,000.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mdogo
wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza Bw. Stephen O'Brien jijini
London, ambapo Uingereza iliahidi kuendelea kuisaidia Tanzania katika
mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kusaidia kuendeleza
sekta ya nishati hususan utafutaji wa gesi asilia.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi akiongea na baadhi ya
wajumbe wa mkutano wa kimataifa wa Uzazi wa Mpango katika ukumbi wa
Queen Elizabeth II jijini London Julai 11, 2012. Kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI), Bi
Josephine Mwankusye na kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Afya ya Mzazi na
Mtoto katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt Neema Rusibamayila.PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)