Mwalimu
wa warembo wa shindano la kumsaka Miss Sinza 2012, Mwajabu Juma, akitoa
maelekezo kwa warembo hao wakati wa mazoezi yao ya mwisho kujiandaa na
shindano hilo litakalofanyika kesho katika Ukumbi wa Mawela Social,
karibu na Vatcan Hoteli, Sinza. Shindano hilo litasindikizwa na burudani
kabambe na shoo ya kufa mtu kutoka kwa Bendi ya African Stars,
watakaokuwa wakitambulisha pia baadhi ya nyimbo zao mpya kwa mara ya
kwanza, pamoja na msanii wa Vichekesho kutoka kundi la Ze Commedy
linalorusha michezo yake kupitia Televisheni ya Chanel 5, Masawe Mtata,
ambaye pia atakuwa akitambulisha video ya wimbo wake mpya uitwao Uongo
Kweli.
Warembo
hao wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja ya shoo ya ufunguzi, jana jioni
ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea shindano lao
litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mawela Social, karibu na Vatcan
Hotel.
Warembo
hao wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja ya shoo ya ufunguzi, jana jioni
ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea shindano lao
litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mawela Social, karibu na Vatcan
Hotel.
Warembo
hao wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja ya shoo ya ufunguzi, jana jioni
ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea shindano lao
litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mawela Social, karibu na Vatcan
Hotel.
Warembo hao wakipozi kwa picha ya pamoja baada ya kumaliza mazoezi yao.
Warembo hao wakipozi kwa picha ya pamoja baada ya kumaliza mazoezi yao.
**********************************
*Mrembo wa Sinza kupatikana kesho (Ijumaa)
Mwandishi Wetu
MASHINDANO
ya kumsaka mrembo bora waKitongoji cha Sinza, Redds Miss Sinza 2012
yatafanyika kesho (Ijumaa) kwenye ukumbi wa Mawela Social Hall (Ten Star
Lounge) uliopo karibu na hoteli ya Vatican City.
Mashindano
hayo yatashirikisha jumla ya warembo 14 wanaowania taji la kituo hicho
pamoja na kuiwakilisha kitongoji cha Sinza kwenye mashindano ya Kanda ya
Kinondoni na baadaye Miss Tanzania.
Mbali
ya taji (crown) na nafasi ya kuiwakilisha Sinza katika Mashindano ya
Kanda ya Kinondoni, pia mshindi wa kwanza katika shindano hilo
atajinyakulia kitita cha sh. 500,000/= katika mashindano hayo
yatakayopambwa na bendi ya African Stars “Twanga Pepeta International’
ambao watakuwa wakitambulisha baadhi ya nyimbo zao mpya na Msanii wa
vichekesho wa kundi la Ze Comedy la Chanel 5, Masawe Mtata, atakayekuwa
akitambulisha video na wimbo wake mpya wa Uongo Kweli.
Akizungumza
na mtandao huu, Mratibu wa mashindano hayo kutoka kampuni ya Calapy
Entertainment, Majuto Omary, alizitaja zawadi nyingine kuwa ni shs
400,000 kwa mshindi wa pili, sh. 300,000 kwa mshindi wa tatu . Mshindi
wa nne na wa tano watapata sh. 150,000 kila mmoja na waliobaki watapata
sh. 100,000 kila mmoja kama kifuta jasho.
Aidha
Majuto, aliongeza kuwa mbali ya kutembea jukwaani kwa ‘catwalk’ kwa
warembo hao, pia kutakuwa na shindano la kusaka vipaji ambapo warembo
watachuana ili kumpata Mafoto Miss Talent Sinza 2012, ambapo mshindi
atapata sh. 50,000 kutoka mtandao wa sufianimafoto.blogspot.com.
“Maandalizi
yamekamilika na viingilio vitakuwa ni sh. 10,000 kwa viti vya kawaida
na sh. 25,000 kwa vitu Maalum (VIP), tumeandaa shoo fupi na ya aina yake
ili baadaye mashabiki wa fani ya urembo wa kitongoji cha Sinza wapate
fursa ya kusugua kisigino na bendi ya Twanga Pepeta,” alisema Majuto.
Majuto
aliwataja Warembo wanaowania taji hilo kuwa ni pamoja na Mariam Miraji,
Naima Mohamed, Lulu Ambonela, Maria John, Judith Sangu, Eva Mushi,
Vailet John na Esther Mussa.
Warembo wengine ni Christina Samwel, Nahma Said, Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi, Brigitter Alfred na Merina Mushi.
Shindano
hilo limedhaminiwa na Redds Premium Cold, Dodoma Wine, Gland Villa
Hotel, Clouds FM, mtandao wa sufianimafoto.blogspot.com, Brake Point,
Fredito Entertainment, Screen Masters, Lady Pepeta na flexi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)