Mwanamuziki
Christian Bella wa bendi ya Akudo Impact katikati akiongozana na
wenzake wakatika wachezaji hao waliposawzisha goli lao, katika mchezo wa
wanamuziki na waigizaji unaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar
es salaa leo, ili kuchangia wahanga wa mafuriko yaliotokea hivi
karibuni jijini Dar es salaam na kusababisha vifo na uharibifu wa mali,
mgeni wa heshima katika pambano hilo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Meck Sadik. Mpaka sasa ni ni kipindina tayari timu ya Bongo Movie
yaani waigizaji wameshajipatia goli la pili hivyo kufanya kuongoza kwa
magoli 2-1 dhidi ya timu ya Wanamuziki na mpia unaendelea.
Mwanamuziki
wa FM Academia Totoo Kalala akiukokota mpira kiuelekea goli la timu ya
waigizaji wakati chezo huo ukiendelea kwenye uwanja wa Taifa.
Hili
ndiyo benchi la ufundi la timu ya Bongo Movie likogozwa na Mzee Chilo
kushoto, JB Steven, Saimon Mwakifwamba na Cheki Budi.
Benchi
la ufundi la Wanamuziki likiongozwa na Asha Baraka wa tatu kutoka
kulia waliosimama na kulia ni MCD wa Twanga Pepeta, Yelo Masai wa FM
Academia na kushoto ni Jose Mara wa Mapacha Watatu wakiwa pamoja na
wachezaji na baadhi ya wanenguaji wa bendi tofauti.Picha Na Father Kidevu Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)