WIMBI la kuuawa madereva wa pikipiki linazidi kushika kasi mkoani
Morogoro ambapo usiku wa kuamkia leo dereva mwingine wa usafiri huo
ambao unajulikana kama ‘bodaboda’ aliyefahamika kwa jina moja la Kasto,
ameuawa kikatili kisha kuporwa pikipiki yake, kunyofolewa macho na
kutupwa kwenye mashamba ya eneo la Chamwino katika Manispaa ya Morogoro.
Mtandao huu ulifika eneo la tukio na kushuhudia umati wa watu
wakiwemo wanafunzi wa shule ya msingi wakijaribu kumtambua marehemu huyo
ambapo baadhi ya watu walimtambua kwa jina la Kasto wakisema alikuwa
akifanya biashara hiyo ya bodaboda kwenye kijiwe cha Tupendane jirani na
nyumbani kwa aliyekuwa mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP) Omar
Mahita.
Wauaji wa mtu huyo waliyanyofoa macho yake kwa lengo la kupoteza
ushahidi wakihofia wangeweza kuonekana kwenye mboni za marehemu huyo.
Takribani mwezi mmoja uliopita dereva mwingine wa bodaboda aliuwawa
kikatili na kuporwa kipikiki yake maeneo ya Kichangani katika Manispaa
ya Morogoro.
NA DUNSTAN SHEKIDELE, MOROGORO
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)