LICHA ya bunge kupandisha bei ya pombe wiki hii, jana majira ya saa
saba usiku mwandishi wa mtandao huu alimnasa mzee mmoja maarufu katika
Manispaa ya Morogoro anayefahamika kwa jina la Sunday akiwa “amezimika”
baada ya kudaiwa kufakamia pombe kwa wingi.
Mwadishi wetu ambaye alikuwa kwenye pilkapilka zake za kusaka
matukio mbalimbali alimkuta mzee huyo usiku huyo mnene kwenye mzunguko
wa magari barabarani mjini Morogoro jirani na stendi ya daladala.
Baada ya kumpiga picha kadhaa akiwa hoi, mwandishi wetu alifanya
jitihada za kumuamsha lakini kutokana na kuzidiwa na kilevi mzee huyo
alishindwa kuzinduka licha ya ubaridi mkali uliokuwepo.
Ili kuepusha wahuni wasimdhuru, mtandao huu ulifanya kazi ya ziada
ya kumuona mlinzi wa kituo cha mafuta kilicho jirani na eneo hilo ili
amsitiri hapo.
NA DUNSTAN SHEKIDELE,GPL MOROGORO
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)