Meneja
Masoko wa TBL,Mamongae Mahlare,Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscer
Shelikindo,Jaji Mkuu wa Shindano Safari Lager Nyama Choma,Lawrence Salvi
pamoja na mpiga picha wa TBC,Jane John walila nyama choma ikiwa ni
sehemu ya uzinduzi wa shindano hilo uliofanyika leo jijini Dar es
Salaam.
Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imezindua
rasmi yale mashindano ya aina yake na ya kuvutia ya kuchoma nyama
yajulikanayo kama “Safari Lager Nyama Choma”
Mashindano haya hushirikisha majiko ya baa mbalimbali katika umahiri wa kuchoma nyama na hatimaye zawadi hutolewa kwa washindi.
Akizungumza
katika uzinduzi wa mashindano ya mwaka huu, meneja wa Bia ya Safari
Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema madhumuni makubwa kwa bia ya Safari
lager kuendesha mashindano haya ambayo yamekuwa kivutio kwa walaji wa
nyama na watumiaji wa bia ni kuhakikisha tunaleta changamoto kwa majiko
yanayochoma nyama, ili kuhakikisha walaji wanapata kile kilicho bora
kabisa.
Watumiaji
wa bia ya Safari Lager, hupendelea sana kuitumia huku wakisindikiza na
nyama choma iliyoandaliwa vizuri, hivyo kupitia mashindano haya, bia
ya Safari Lager inaendeleza utamaduni wa kunywa bia na kula nyama.
Kufuatia ubora wa hali ya juu wa bia ya Safari lager, tunafurahi sana
pale ambapo mnywaji atapata pia nyama iliyo bora ili mtumiaji aweze
kuridhika zaidi.
Mashindano
ya mwaka huu yatafanyika katika mikoa mitano ambayo ni; Dar Es Salaam,
Kilimanjaro, Arusha,Mbeya.na Mwanza. Kuna ongezeko la mkoa wa Mwanza
ambao mwaka juzi haukushiriki. Ni matarajio ya bia ya Safari Lager
kuyapeleka mashindano haya katika mikoa yote siku za usoni.
Akitaja
zawadi za washindi, Shelukindo alisema; baa itakayoshika nafasi ya
kwanza itajinyakulia shilingi Milioni Moja, mshindi wa pili, Laki Nane,
Mshindi wa Tatu laki Sita, Nafasi ya Nne; Laki Nne na nafasi ya Tano
shilingi Laki Mbili. Zawadi hizi zimegawanywa kwa kila mkoa.
Utaratibu
wa kupata baa zitakazoshiriki mashindano haya utaendeshwa kwa njia ya
simu, ambapo wananchi watatakiwa kutuma ujumbe mfupi usemao “Safari
kisha Mkoa uliopo ikifuatiwa na jina la Baa” kisha tuma kwenda namba
0763 514 514 Utapokea ujumbe kukuhakikishia kuwa kura yako imepokelewa.
Jopo
la majaji litapitia kura zote na Baa ishirini kwa Dar Es Salaam na
Kumi kwa mikoa mingine zitakazokuwa zimepata alama za juu zaidi ndizo
zitakazopambana katika hatua ya pili ya tano bora ambapo majaji
watazitembea tena na kutoa maksi kulingana na vigezo waliovyo navyo
kasha baa hizo zitapambana katika eneo la wazi ambapo mandhari ya kula
nyama na kunywa bia itakuwa imeandaliwa.
Kwa Upande wake Jaji mkuu wa Mashindano ya mwaka Douglas Sakibu akizungumzia
Vigezo
vitakavyoangaliwa na majaji katika mashindano haya ni pamoja na Usafi
wa eneo, vifaa na muhusika, uchaguzi wa nyama, maandalizi ya nyama,
jinsi ya uchomaji, muda unaotumika, jinsi nyama inavyofikishwa kwa mlaji
na Ladha. Baa zitakazofanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro zitapewa
semina elekezi juu ya vigezo hivi kabla ya mpambano.
Alisema
hii ni fursa ya pekee kwa wachoma nyama na wenye mabaa kuweza kupata
mafunzo yakinifu juu ya uandaaji na uchomaji wa nyama toka kwa wataalam
wenye ujuzi na waliobobea kwenye taaluma hiyo ili kuweza kukuza na
kuboresha biashara zao na hatimae kufikisha kwa wateja kitu kilichokuwa
na ubora wa hali ya juu.
Mashindano
ya Safari Nyama Choma mwaka huu yanafanyika kwa mara ya nne ambapo
mwaka jana washindi wa Jiji la Dar Es Salaam walikuwa Kisuma Bar ya
Temeke Mwembe Yanga,Mbeya walikuwa Mbeya Canival,Kilimanjaro walikuwa
Makanyaga bar ya Soweto na Arusha walikuwa SongaMbele Bar ya Sakina.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)