Afisa
Masoko Mwandamizi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) katika mikoa
ya Arusha na Manyara Joan Semuguruka akitoa salamu za kampuni hiyo kwa
wafanyakazi wa benki mbalimbali (hawapo pichani) zilizoshiriki hafla
ya 'Bankers Gala Night' iliyofanyika mkoani Arusha mwishoni mwa
wiki.SBL kupitia bia yake ya Tusker Malt ilidhamini hafla hiyo.
Baadhi
ya wafanyakazi wa benki tofauti nchini wakipatiwa utaratibu kabla ya
kuingia katika hafla iliyowakutanisha pamoja wafanyakazi wa benki
katika tukio lililojulikana kama 'Bankers Gala Night'.Tukio hilo
lilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha na kudhaminiwa na Kampuni
ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Tusker Malt.
KAMPUNI
ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Tusker Malt imeahidi
kuendelea kutoa ushirikiano ndani ya sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya
kibenki katika lengo la kukuza maendeleo ya uchumi nchini.
Hii
ilikuwa wakati wa hafla maalum ya wadau katika sekta ya kibenki
iliyodhaminiwa na bia ya Tusker Malt na kuzileta pamoja taasisi za
kifedha zikiwemo benki zinazoongoza kibiashara nchini.
Hafla
hiyo ilifanyika katika Hotel ya Snow Crest jijini Arusha mwishoni mwa
wiki ilitoa fursa maalum kwa wawakilishi wa taasisi mbalimbali za
kibenki kuzungumza pamoja changamoto mbalimbali zinazoikabiri sekta ya
fedha nchini.
Akizungumza
wakati wa halfa, Afisa wa kampuni ya Serengeti wa Nyanda za Juu
Kaskazini, Bw. Mapendo, alisema kuwa kampuni yake itaendelea kufanya
kazi karibu na wadau wote ili kuleta maendeleo ya uchumi nchini.
Alisema
hafla hiyo imetoa nafasi kubwa kwa wadau wa taasisi za kifedha haswa
za kibenki kuungana pamoja na kubadilishana mawazo jinsi gani wanaweza
kusonga mbele na kupanua sekta hiyo muhimu katika uchumi wa taifa.
Mapendo
alisema SBL kupitia kinywaji chake cha Tusker Malt imedhamini hafla
hiyo na kwamba itaendelea kushirikiana na sekta hiyo katika mambo
mbalimbali kulingana na uwezo wake kifedha.
“Sekta ya kibenki inakuwa kwa kasi sana na hivyo kutoa fursa nyingi mbalimbali kwa nyanja zote mbili za kibiashara pamoja na ajira kwa watanzania walio wengi. Na fursa hizo huonekana zaidi wakati wa matukio muhimu kama haya.
"Tunaamini
kwamba kupitia hafla hii, jamii ya wafanyabiashara itachukua na
kuzifanyia kazi fursa zilizopatikana. Tunajivunia kuwa wadhamini wakuu
wa tukio hili.
“Bia
ya Tusker Malt imekuwa ikidhamini matukio mbalimbali nchini lakini
mwaka huu tumedhamiria kuweka mkakati madhubuti ambao unaangalia zaidi
biashara katika makampuni na makundi mengine ndani ya jamii,” aliongeza.
Kwa
upande wake mwakilishi wa waandaaji wa tukio hilo Peter Morgan
aliishukuru Tusker Malt kwa udhamini wake na kusema kuwa ni vyema SBL
ikaendeleza wazo hilo zuri la kuwa na matukio kama hayo katika kanda
mbalimbali nchini.
“Hili
ni tukio la kukumbukwa ndani ya jamii ya wadau wa taasisi za kibenki.
Tumeweza kuzikutanisha taasisi mbalimbali za kifedha pamoja si kukutana
tu bali pia kuweza kubadilishana mawazo jinsi ya kutatua changamoto
mbalimbali zinazoikabiri sekta ya kibenki. Tunaishukuru bia ya Tusker
Malt kwa udhamini wake,” alisema.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)