Watanzania Waishio Nchini Uingereza Wachangia Waathirika na Mafuriko Jijini Dar es Salaam - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Watanzania Waishio Nchini Uingereza Wachangia Waathirika na Mafuriko Jijini Dar es Salaam

Hivi ni baadhi ya vitu vilivyo patikana katika Harambee.
Mzee wa Kazi Chris Lukosi akiwajibika.
Chris, jestina na wadau wengine wakikusanya misaada mbalimbali.
Wadau waliojitokeza kufanikisha harambee wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni Rasmi Mh. Naibu Balozi Chabaka Kilumanga.
--
salaam,

Siku ya jumamosi tarehe 7 January 2011 Serengeti freight wakishirikiana na Miss Jestina Blog pamoja na Urban Pulse walifanya harambee maalum ya kuchangia watanzania walioathirika na mafuriko yaliotokea hivi karibuni mwishoni mwa mwaka jana  nyumbani Tanzania.

Mgeni rasmi alikuwa Naibu balozi Mh Chabaka Kilumanga.  Aidha Mh Balozi aliongea na kushukuru watanzania wote walioguswa na kujitolea kwa hali na mali ili kuweza kusaidia watanzania wenzao waliokumbwa na janga hili. Misaada bado inaendelea kupokelewa na kukusanywa mpaka mwisho wa mwezi huu wa january. Hivyo basi kwa wale wote walioshindwa kuweza kufika siku ya jumamosi kutoa michango bado  nafasi ipo. Kumbuka hili ni janga letu wote tafadhali fanya sehemu yako kwa jinsi Mungu anavyokubariki. 

KWA MAWASILIANO ZAIDI KUHUSU MISAADA WASILIANA NA
JESTINA GEORGE 07404332910
FRANK  EYEMBE 07865594576
BARAKA NYAMA 07816981577 
 
KAMA UNA MCHANGO UNAWEZA KUDEPOSIT KATIKA ACCOUNT IFUATAYO:
BARCLAYS BANK
JINA: TANZANIA ASSOCIATION LONDON Account Number: 23374815 
Sort Code: 20-72-89 
ANDIKA JINA LAKO NA MAFURIKO AS REFERENCE
 
TUNAWASHUKURU NYOTE KWA KUJALI NDUGU ZETU
Contact us for more info;
CHRIS LUKOSI 07903828119 
SIMON LOUIS (MOHSIN) 07950689243
BRIAN (BABA NJOROGE) 07795160757
HASSAN (RICHARD) 07405159255
HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH

Asanteni sana kwa kuonesha moyo wa Kiuzalendo. 

MUNGU AWABARIKI,

Serengeti Freight, Miss Jestina Blog na Urban Pulse

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages