Mhariri Mtendaji wa magazeti ya MwanaHALISI na Mseto, Saed Kubenea Afanyiwa tena Upasuaji Wa Macho Nchini india - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mhariri Mtendaji wa magazeti ya MwanaHALISI na Mseto, Saed Kubenea Afanyiwa tena Upasuaji Wa Macho Nchini india

  Mtendaji mkuu wa magazeti ya Mwanahalisi, Saed Kubenea akiwa katika baskeli ya wagonjwa kwenye hospitali Apollo iliyopo New Delhi nchi India anakotibiwa ugonjwa wa macho. Kubenea. yuko hospitalini tangu Jumanne iliyopita na tayari amefanyiwa upuaji wa macho yake yote mawili jana. Ameekuwa akitibiwa kwenye hospitali hiyo tangu mwaka 2008 baada ya kumwagiwa tindakali ofisini kwake, Kinondoni Dar es Salaam
Mhariri Mtendaji wa magazeti ya MwanaHALISI na Mseto, Saed Kubenea akichukuliwa vipimo na mmoja wa wahudumu wa hospitali ya Apollo nchini India kabla ya kupelekwa kwenye chumba cha upasuaji . Kubenea yuko nchini India kwa matibabu ya macho yalitotokana na kumwagiwa tindikali. Tayari amefanya upasuaji huo jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hali halisi publishers Ltd, Saed Kubenea akiwa katika  wodi ya Hospitali ya Apollo, New Delhinchi INDIA mara baada ya kufanyiwa  Upasuaji macho jana.Kubenea amekuwa akitibiwa katika Hospitali hiyo tokea mwaka 2008 alipomwagiwa tindikali katika ofisi yake jijini Dar es Salaam na hii ni operesheni yake ya tano.Picha zote kwa hisani ya  Abdulkarim Hussen.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages