Muandaaji
Wa Fashion For Floods Mustafa Hassanali akiongea na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo.wa Pili kushoto ni Mayor Wa Manispaa ya Ilala
Jerry Silaa,Ailena Mhanga,Hamis K.Omary
Senior
Sales Manager wa Serena Hotel,Ailena Mhanga, akiongea na waandishi wa
habari juu ya Fashion For Floods kulia kwake ni Marketing manager wa 361
degrees ,Hamis K.Omary
Muandaaji
wa Fashion For Flood Mayor wa Ilala .Jerry Silaa akiongea na waandishi
wa habari leo Kulia kwake ni Senior sales Manager Serena Ailena
Mhanga na Hamis K.Omary
---
MUSTAFA HASSANALI AKIUNGANA NA MEYA WA MANISPAA YA ILALA MH. JERRY SILAA KUCHANGISHA PESA YA KUSAIDIA WAHANGA WA MAFURIKO DAR-ES-SALAAM
MAONYESHO YA KWANZA YA MITINDO KUCHANGISHA PESA KWA AJII YA KUSAIDIA WAHANGA WA MAFURIKO
MITINDO KWA AJII YA MAFURIKO ITAFANYIKA KATIKA HOTELI YA SERENA TAREHE 12-JAN-2012
Mbunifu wa kiafrika Mustafa Hassanali na Meya wa manispaa ya ilala Mh.Jerry Silaa wameungana
kwa pamoja ili kuchangisha pesa kwa ajii yakuwasaidia watanzania
waliokumbwa na janga la mafuriko lilosababishwa na mfululizo wa mvua
kubwa ivi karibuni December 2011 jijini Dar es Salaam.
Maonyesho
ya mitindo ya kwanza nchini Tanzania kufanyika kwa ajili ya kuchangisha
pesa za kuwasaidia wahanga wa mafuriko,ambayo yatafanyika Alhamisi tarehe 12 Januari 2012 katika hoteli ya Serena Dar es Salaam. Mustafa Hassanali ataonyesha ubunifu wake uliokubalika kimataifa kuanzia Johannesburg mpaka Stockholm,katika tukio hili tutaona wanamtindo wakitanzania wakiudhibitisha ubunifu wake.
“Nimeguswa
sana na tatizo hili lilowakumba watanzania wenzetu, na kwa namna moja
au nyingine wote tumeadhirika na tatizo hili. Ndo kwasababu mimi na Meya
tumeamua kusaidia kwa kuandaa hafla ya kuchangisha pesa ya kuwasidia wahanga hawa”. Alisema Mustafa Hassanali
Mafuriko haya yameadhiri nchi nzima
kiujumla, Mamia ya watu walokumbwa na janga hili la mafuriko hawana
makazi ya kudumu na wengi wao wakiwa wanategemea misaada kama hii ili
kujikimu katika mahitaji yao ya kila siku.
“Nngependa kuwahamasisha watu wengi waloguswa na tatizo hili kuhudhuria katika maonyesho haya ili kuweza
kuwa mmoja kati ya watu watakaowasaidia na kuwafariji wahanga hawa wa
mafuriko kwa kushirikana pamoja na kuleta mabadiliko katika maisha yao
.” Alimalizia Hassanali.
Mitindo
kwa ajili ya mafuriko yatafanyika katika hoteli ya Serena tarehe
12-Jan-2012 kuanzia saa 2:30 usiku, kiingilio ni shillingi 25,000 kwa
viti vya kawaida na 50,000 kwa viti maalum . Maonyesho haya yamedhaminiwa
na Serena Hotels Dar es Salaam, Clouds FM, Clouds TV, Vayle Springs,
Event Lites, Darling Hair, H-Models, Samaki Samaki, Rockers night club,
24HR Media na 361 Degrees.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)