Ni Kusanyiko La Magezi-gezi? Wakufunzi Wa Wakufunzi Wa Wanahabari Wakutana Morogoro - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Ni Kusanyiko La Magezi-gezi? Wakufunzi Wa Wakufunzi Wa Wanahabari Wakutana Morogoro

Ndugu zangu, 

Moyo wangu ulidunda, mara ile nilipopokea na kusoma mwaliko wa kujumuika na kusanyiko la wanahabari waliobobea na wenye majina makubwa.  Ni kwenye mafunzo ya wakufunzi wa wanahabari. 


Kaka yangu Kajubi Mukajanga anasema; Wahaya wanamwita mtu anayejifanya anayejua jua sana mambo kwa jina la ' Lugezi-gezi'- Kwamba yeye anajua kila kitu!"


Nami nilidhani ningefika Morogoro na kukutana na watu wenye hulka ya 'lugezi-gezi'- wajuaji wa kila kitu. Kwamba nisingekuwa na kipya cha kuwaambia. 


HAPANA!

Kusanyiko hili la Morogoro limeniondoa mashaka hayo. Kila mmoja anaonekana kuwa na utayari wa kujifunza kutoka kwa mwenziye. Kuna utani mwingi pia. Tunacheka sana. Tunajifunza.

Naam, kusanyiko la Morogoro lina  waandishi wenye uzoefu wa miaka mingi  kwenye tasnia ya habari. Kuna majina kama Kajubi Mukajanga, Fili Karashani, Aboubakar Karsan, Nyaronyo  Kicheere, Allan Lawa, Ally Saleh, Said Dogoli, Deo Mfugale, Moses Mataba, Mnaku Mbani.... orodha kamili inakuja.

Maggid Mjengwa,
Morogoro.
Ijumaa, Januari 6, 2012.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages