JESHI la Polisi nchini limekipongeza Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) kwa kuonyesha ukomavu wake kisiasa kulikodhihirishwa
na kitendo chake cha mchango wa sh 200,000 za rambirambi kwa ajili ya
askari Kijanda Mwandu mwanzoni mwa wiki iliyopita mkoani Arusha.
Akipokea mchango huo wa rambirambi kutoka kwa viongozi wa CHADEMA, mkoa wa Arusha, jana, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi hilo, Saidi Mwema, Kamanda wa Polisi wa mkoa, Thobias Andengenye, alisema kitendo cha CHADEMA kujitokeza na kushiriki nao katika msiba wa askari wake, kitafungua upya ukurasa wa mshikamano baina ya pande hizo mbili.
Kamanda Andengenye alisema pamoja na polisi kufarijika kwa kitendo cha CHADEMA kuungana na familia, ndugu na jamaa wa marehemu, hatua hiyo imedhihirisha kuwa jeshi hilo na marehemu Mwandu wanajituma kuwatumikia wananchi kwa moyo na kwamba hakuna chuki baina ya pande hizo mbili.
“Licha ya tukio hilo kudhihirisha kuwa makundi mbalimbali ya kijamii yanatambua na kuthamini mchango na umahiri wa marehemu kiutendaji wakati wa uhai wake, jambo kubwa ambalo litafungua ukurasa mpya kati ya polisi na CHADEMA ni kwamba mchango huu umedhihirisha kwamba hakuna chuki wala uhasama kati ya jeshi letu na chama hiki kikuu cha upinzani kama watu wengine wanavyofikiri,” alisema Kamanda Andengenye.
Alifafanua kuwa wakati mwingine polisi na CHADEMA wamekuwa wakihitilafiana katika utekelezaji wa harakati, shughuli zao za kila siku na usimamizi wa sheria ambapo wakati mwingine hujikuta wakikabiliana bila kukusudia.
Kamanda Andengenye alisema fedha hizo zitaandikiwa taarifa na kuwasilishwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Saidi Mwema, ambaye atapanga utaratibu wa kuzifikisha kwa familia ya marehemu Kijanda Mwandu aliyezikwa nyumbani kwao Magu, mkoani Mwanza, wiki iliyopita.
Msafara wa viongozi wanne wa CHADEMA waliokabidhi ubani huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Wilaya ya Arusha, Ephata Nanyaro, aliyeongozana na Mwenyekiti wa Madiwani wa CHADEMA katika Baraza la Madiwani Manispaa ya Arusha, Isaya Doita; Mwenyekiti wa Baraza la wanawake (Bawacha), wilaya ya Arusha, Gloria Shio; na mjumbe wa Kamati ya Utendaji wilaya, Sarah Fundikira ambao kwa pamoja walielezea kusikitishwa na kifo cha askari huyo aliyejitolea maisha yake kupambana na kudhibiti uhalifu.
Nanyaro ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Levolosi alisema CHADEMA kama wadau wa amani, utulivu na ulinzi wa raia na mali zao mkoani Arusha, wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha askari huyo pamoja na kujeruhiwa kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Faustine Mafwele, katika tukio lililotokea Januari 3, mwaka huu, eneo la Shangarai, wilayani Arumeru.
“Fedha hizi kidogo ni mchango wa viongozi, wanachama, wapenzi wa CHADEMA na wananchi waliohudhuria mkutano wetu wa hadhara kuadhimisha kumbukumbu ya waliouawa na kujeruhiwa katika tukio la maandamano ya Januari 5, mwaka jana,” alisema Nanyaro.
SOURCE:TANZANIA DAIMA

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)