Airtel Money yaongeza wakala, sasa ni zaidi ya 10,000 tangu kuzinduliwa - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Airtel Money yaongeza wakala, sasa ni zaidi ya 10,000 tangu kuzinduliwa

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mhe. Mustafa Mkulo (wa pili kulia) alipokuwa akizindua huduma ya Airtel Money akiwa na Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Sam Elangalloor na Mkurugenzi wa Airtel Money, Kelvin Twissa (kulia) ikiwa ni mwezi mmoja sasa umepita.
Mkurugenzi wa Airtel Money, Kelvin Twissa akiongea na wanahabari (hawapo pichani).
Wakala wa Airtel Money anaefanya kazi usiku na mchana katika fukwe maarufu ya Coco Beach, Peter Makundi akiwa kazini.
Watoa huduma hawa wanapatikana sehemu mbalimbali kutoa elimu jinsi ya kutumia orodha mpya ya Airtel Money kama mabango yanavyoonyesha hapo nyuma yao.
. Airtel yaendelea kuzalisha ajira kupitia huduma ya Airtel Money.

. Kupanuka kwa mtandao wa Airtel sambamba na ongezeko la WAKALA wa Airtel Money kunaleta maendelea kwa wakazi wa mjini na vijijini.


Huduma ya Airtel Money ambayo  awali ilijulikana kama ZAP, sasa ni moja kati ya huduma inayoendelea kuenea huku ikineemesha baadhi ya wajasiriamali wadogo wadogo nchini Tanzania kwa kuongeza wigo wa ajira na kipato katika shughuli zao.


Airtel Money ni huduma ya kibenki kupitia simu za mkononi ambapo inatolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel yenye mtandao mpana na ulioenea zaidi katika maeneo ya mjini na vijijini.


Akingea na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Airtel Money, Bw. Kelvin Twissa, alisema "Huduma ya kutuma na kupokea pesa kupitia simu ya mkononi ya Airtel inajulikana kama Airtel Money, huduma hii ya kutuma na kupokea pesa kupitia simu yako ya kiganjani kwa sasa imekuwa ni moja ya sehemu ya mfumo wa maisha ya kila siku kwa watumiaji  nchi nzima,  hususani kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.


Tangu tulipozindua huduma hii kuwa  Airtel Money mwishoni mwa mwaka jana, leo hii tayari imetimiza zaidi ya Wakala 10,000 (elfu kumi) waliosambaa nchi nzima katika maduka madogo madogo pamoja na wale wafanyabiashara wa kati ambao kwa hali ya kawaida wamejiajiri na tayari wameshaanza kutengeneza faida kubwa kutokana na ile kamisheni wanayoipata kila wanapotoa huduma hii kwa wateja wetu. Airtel Money ni huduma ambayo ni rahisi na inakidhi mahitaji ya watu wa rika zote katika mifumo yote ya uhamishaji wa fedha."


Mfano mzuri ni kama mtu akitaka kuhamisha fedha kupitia njia zozote za kawaida ni lazima asafiri umbali wa kilometa 50, kuja au kwenda katika makao makuu ya wilaya yake ili akutane na watoa huduma ili atume  au kupokea fedha katika njia za kawaida tulizozoea awali, lakini sasa huduma hii  ya kibenki kupitia simu ya mkononi ya Airtel Money hasa vijijini inaweza kufikiwa kwa umbali wa kila kilometa moja unakutana na DUKA lenye wakala, ndio maana leo tunaona fahari kuwa na zaidi ya mawakala 10,000 muda mfupi toka tulipoizindua huduma hii ya Airtel Money.


Twissa alisisitiza "huduma hii pia inalenga zaidi Watanzania wanaoishi vijijini na mijini hususani sehemu ambazo kampuni ya Airtel imepanua wigo kwa kuzindua mawasiliano mapya kwa kuwa hakuna mtandao mwingine unaopatikana. Airtel Tanzania bado inaendelea na mkakati wa kuweka miundo mbinu ya mawasiliano bora katika maeneo ya vijijini sambamba na kuhakikisha huduma hii ya Airtel Money inawafikia wateja wetu walioko kila pande ya nchi yetu na kuwafaidisha.


Airtel Money ni huduma inayowawezesha watumiaji kupokea fedha na kutuma fedha, vili vile inawawezesha kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti zao za benki, aidha kuwatumia muda wa maongezi jamaa zao pamoja na kulipia bili mbalimbali ikiwemo LUKU, DSTV, Dawasco na hata kulipia ada kwa shule mbalimbali zilizokwisha jiunga na mfumo wa ulipaji ada kupitia Airtel Money.


Huduma ya Airtel Money awali ilijulikana kama ZAP na kuzinduliwa kuwa Airtel Money Disemba 6, 2011 ikiwa ni mikakati ya kampuni ya mawasiliano ya Airtel kuboresha na kuongeza huduma zake kwa wateja wake.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages