Vodacom
Miss Tanzania Salha Isarel akipokea funguo ya gari aina ya Jeep
Patriot, kutoka kwa Meneja Matukio na Udhamini wa kampuni ya simu za
mkononi Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa, wakati wa hafla fupi ya makabidhinao ya zawadi ya mrembo huyo aliyetwaa taji la Vodacom Miss Tanzania 2011, katika
shindano la Taifa lililofanyika Septemba. Kulia ni Mkurugenzi wa Lino
Agency waratibu wa shindano hilo la Vodacom Miss Tanzania, Hashim
Lundenga na (kushoto) ni Meneja Masoko wa CFAO wadhamini wenza wa
shindano hilo, Alfred Minja. Gari hiyo ina thamani ya shilingi Milioni 72.
Vodacom
Miss Tanzania Salha Isarel akionyesha funguo ya gari aina ya Jeep
Patriot lenye thamani ya shilingi milioni 72 kwa furaha baada ya
kukabidhiwa na Meneja Udhamni na Matukio wa kampuni ya Vodacom Tanzania
Rukia Mtingwa (wa pili kulia).
Meneja
Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa, akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi
rasmi zawadi ya Vodacom Miss Tanzania 2011, Salha Israel. Kulia ni
Meneja Masoko wa CFAO Alfred Minja ambao ni wadhamini wenza wa shindano
la Vodacom Miss Tanzania.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)