Vikombe vitakavyoshindaniwa kwenye ligi ya kombe la mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Dewji.
Katibu
wa CCM manispaa ya Singida akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa
vya michezo vilivyotolewa na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh.
Mohammed Dewji.
Katibu
wa CCM manispaa ya Singida Magdalena Ndwete akionyesha jezi
zitakazotumiwa wakati wa ligi ya kombe la mbungeMh. Mohammed Dewji.
Msaidizi
wa mbunge Mohammed Dewji Duda Mughenyi akishiriki kugawa vifaa vya
michezo kwa ajili ya ligi ya Mo.Picha zote na Nathaniel Limu
---
Na.Nathaniel Limu.
Ligi
maarufu ya kombe la mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed
Gullam Dewji inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 18/12/2011
kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida.
Kwa
mujibu wa mratibu wa ligi hiyo Katibu wa mbunge Dewji Duda Mughenyi,
jumla ya timu 16 za soka za kata ya Manispaa ya Singida zitashiriki ligi
hiyo.
Duda
amesema Mh. Dewji ametoa jezi 240, mipira 53 na soksi 240 ambapo kila
kata imepata jezi pea 15 na soksi 15 kwa ajili ya kufanikisha maandalizi
ya kushiriki ligi.
Amesema
timu hizo za kata ambazo hazina chembe chembe yo yote ya itikadi ya
kisiasa, udini, ukabila, wala rangi, zimegawanywa katika makundi manne
ambapo kila kundi litakuwa na timu nne.
Duda
amesema kundi A, litakuwa na timu za kata ya Mitunduruni, Ipembe,
Utemini na Minga, Kundi B, Majengo, Kindai, Mughanga na Misuna, Kundi C,
Unyambwa, Mandewa, Mtipa na Uhamaka na kundi D, Litakuwa na timu ya
kata ya Mtamaa, Mungumaji, Unyamikumbi na Mwankoko.
Amesema
ligi hiyo inayotarajiwa kumalizika Januari 21 mwakani, mechi ya fungua
dimba ambayo itachezwa Jumapili Desemba 18 mwaka huu, itazikutanisha
timu za Mitunduruni na Utemini.
"Mshindi
wa kwanza, atapata kombe kubwa hadhi ya dhahabu na shilingi laki moja
taslimu, wa pili atapata kombe dogo na shilingi laki mbili, wakati yule
wa tatu, atazawadiwa shilingi laki moja", amesema Duda.
Akizungumza
kenye hafla ya kugawa vifaa vya michezo ya ligi hiyo, Katibu mpya wa
CCM Manispaa ya Singida, Magdalena Ndwete, amewataka wachezaji wa timu
hizo, kuheshimu sheria 17 za soka, ili kudumisha amani na utulivu wakati
wote wa ligi hiyo.
"Mkifanya
hivyo, lengo la mbunge wetu Dewji la kukuza vipaji vyenu, kuwasaidia
kujitangaza, kujenga afya na kupanua wigo wa marafiki, litafikiwa kwa
ufanisi mkubwa” amesema.
Kwa
upande wa waamuzi wa ligi hiyo, Ndwete, amewataka wasijihusishe na
vitendo vitakavyochangia kuvuruga ligi hiyo vikiwemo vya upendeleo na
uonevu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)