Katibu
wa NEC ya CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipongezwa na mama yake,
Kezia Alfred, baada ya kutunukiwa shahada ya pili ya uongozi katika
mahafali ya kumi ya Chuo Kikuu Mzumbe, leo.
KATIBU
wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto) akijadili
jambo na wahitimu wenzake wa Shahada ya pili ya uongozi, katika
mahafali ya kumi ya Chuo Kikuu Mzumbe, leo kwenye ukumbi wa Diamond
Jubilee, Dar es Salaam. Kutoka wapili kushoto ni, Anedina Hongele, Zakia
Omari, Magnus Mahenge na Meja Joseph Masanja.
Watangazaji
wa Kituo cha Televisheni cha Chanel Ten Fredy Mwanjala, Salama Hamadi
na Zainab Abdul, wakimpa zawadi ya hongera, Katibu wa NEC, Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye ambaye ametunukiwa shahada ya pili ya uongozi leo
kwenye mahafali ya kumi ya Chuo Kikuu Mzumbe, kwenye ukumbi wa Diamond
Jubilee, Dar es Salaam.
Nape akipongezwa na baba yake mdogo, Mzee Galus Abeid katika mahafali hayo. Katikati ni mama wa Nape, Kezia Alfred.
Nape akipongezana na mhitimu mwenzake kwenye mahafali hayo, Wilfred
Gallaba ambaye ni Mkaguzi wa hesabu Ofisi ya Ukaguzi ya Taifa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)