BENKI YA NBC YAZINDUA KITUO CHA KUTOA HUDUMA KWA WATEJA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BENKI YA NBC YAZINDUA KITUO CHA KUTOA HUDUMA KWA WATEJA

Mkurugenzi wa Benki ya NBC Bw. Rawlence Mafuru akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha huduma kwa wateja cha benki ya NBC uliofanyika kwenye ukumbi wa benki hiyo iliyopo Mtaa wa barabara ya Sokoine jijini Dar es salaam, wanaoshuhudia tukio hilo kulia ni Jane Dogani Meneja Huduma kwa wateja, kutoka kulia ni Maharage Chande Ofisa Mwendeshaji Mkuu na NBC na Ngitika Meneja wa kituo cha Mawasiliano Huduma kwa wateja. 

Mkurugenzi wa Benki ya NBC Rawlence Mafuru akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa benki hiyo leo wakati alipozinduz rasmi Kituo cha kutoka Huduma kwa wateja NBC Contact Centre) kikiwa na lengo la kuboresha mitazamo na uzoefu wa wateja kwa benki hiyo kote nchini Kushoto ni Ngwitika Mwakahesya Meneja wa Kituo cha Mawasiliano huduma kwa Wateja.
Mkurugenzi wa Benki ya NBC Rawlence Mafuru kulia akizungumza na Maharage Chande Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC mara baada ya kuzidua rasmi kituo cha huduma kwa wateja cha benki hiyo.
Wafanyakazi mabalimbali nao wamejumuika katika uzinduzi huo.
Wafanyakazi mabalimbali nao wamejumuika katika uzinduzi huo.
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) inafuraha kubwa kutangaza uzinduzi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja (NBC Contact Centre) kikiwa na lengo la kuboresha mitazamo na uzoefu wa wateja kwa benki hiyo. 

Katika mkakati huo, hoja, maswali, matatizo na ushauri mbalimbali wa wateja vitakusanywa, vitafuatiliwa na kufanyiwa kazi ili kuhakikisha kuwa kunakuwapo na kiwango cha juu kabisa cha uwajibikaji, umiliki na uwazi. Mkondo huu mpya kwa wateja wa NBC umetengenezwa makusudi ili kuweka wazi changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wateja wa NBC. Benki hii inajitahidi kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na wateja wake.

Katika kuhakikisha kuwa hatua hii mpya inaleta mafanikio chanya kwa NBC, benki imeweka mfumo bora wa huduma kwa wateja utakaowaruhusu mawakala wa NBC wa huduma kwa wateja kuzishughulikia ipasavyo simu zote au hoja zote zitakazopelekwa na wateja hivyo kuleta uhusiano mwema kati ya benki na wateja wake. Mawakala wote wamefundishwa kushughulikia miito ya hoja (za simu) kwa weledi wa hali ya juu, upendo na kwa kasi. Kwa kuanzia, NBC imetengeneza line nne ambazo ni; huduma za kibenki, huduma za ATM, huduma za kadi za benki na Masuala ya Mikopo. 

NBC ingependa kuchukua nafasi hii kuufahamisha umma kwamba Kituo cha huduma kwa wateja cha NBC kiko wazi na tayari kabisa kukuhudumia na kuwaambia wateja wetu wa sasa na wa baadaye wawe huru kutumia huduma hizi kupitia namba za simu 0768984000, 0225511000 na 0222193000.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages