ASANTE KOTOKO YAITUNGUA SIMBA 1-0 UWANJA WA TAIFA LAKINI YAONYESHA KIWANGO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

ASANTE KOTOKO YAITUNGUA SIMBA 1-0 UWANJA WA TAIFA LAKINI YAONYESHA KIWANGO

Wachezaji wa timu ya Simba wa wakichuana vikali na mchezaji wa Asante Kotoko ya Ghana katika mchezo wa kirafiki unaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni hii , Asante Kotoko imefanikiwakuifunga Simba katika kipindi cha pili goli 1-0 huku Simba ikio ambayo ilichezesha kikosi cha pili ikionyesha uwezo mkubwa katika mchezo huo jambo lililowafanya mashabiki kuwashangilia wachezaji hao baada ya mpira kumalizika, lengo la mchezo huo ni kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania
Wachezaji wa Asante Kotoko na Simba wakitibiwa mara baada ya kugogana na kuumia katika purukushani za kuwania mpira uwanjani.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la NSSF Bw. Crescentius Magori akisalimiana na wachezaji wa timu ya Asante Kotoko ya Ghana kabla ya kuanza kwa mchezo uwanja wa Taifa
Kikosi cha timu ya Simba kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Kikosi cha timu ya Asante Kotoko kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo. Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la NSSF Bw. Crescentius Magori kulia akiongoza na na viongozi wa Simba na Asante Kotoko kwenda kukagua timu.Picha na Full Shangwe Blogu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages