Sherehe Za Miaka 50 Ya Uhuru Zafana Roma - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Sherehe Za Miaka 50 Ya Uhuru Zafana Roma





Ile sherehe ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara  ambayo ilikuwa inasubiliwa na Watanzania wote nchini Italy, ilifanyika siku ya ijumaa tarehe 9 Disemba 2011. Sherehe ilipambwa na Watanzania kutoka sehemu mbalimbali za Italy kama vile Rome, Modena, Napoli, Siena na sehemu zingine na pia kuudhuliwa na wageni kadhaa kutoka nchi rafiki za Tanzania. Mgeni wa heshima alikuwa Kaimu Balozi, Mh. SalvatorI Mbilinyi ambaye aliambatana na maafisa wote wa ubalozi wa Tanzania nchini Italy. Sherehe ilianza kwa kuimba wimbo wa Taifa na baadae mgeni waheshima Kaimu Balozi Mh. Salvator Mbilinyi kuIfungua rasmi. Kaimu balozi alianza kwanza kwa kuelezea umuhimu wa kusherekea siku hii ya miaka 50 ya uhuru na baadae kuelelezea kistoria jinsi gani Tanzania ilipata uhuru kutoka kwa wakoloni wa kiingereza. Mh. Kaimu balozi aliwashukuru pia Watanzania wote kwa ushirikiano wao walioonyeshe kwenye kuiandaa siku hii muhimu. Aliwashukuru zaidi viongozi wa jumuiya mbali mbali za kitanzania hapa Italy kwa ushirikiano waliouonyesha kwenye maandalizi ya sherehe hii. Mungu Ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages