ZIARA YA PRINCE OF WALES HUKO ARUSHA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

ZIARA YA PRINCE OF WALES HUKO ARUSHA

The Prince of Wales na The Duchess of Cornwall wakiangalia ngoma ya mganda mara tu baada ya wageni hao kuwasiri kwenye uwanja wa ndege wa Kilimanjaro katika ziara yao ya siku moja mkoani Arusha tarehe 9.11.2011.
The Prince of Wales na The Duchess of Cornwall wakikaribishwa kwa ngoma za kimasai wakati walipowasiri katika kijiji cha Majengo kilichoko wilayani Arumeru kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na Uingereza.

The Prince of Wales na The Duchess of Cornwall wakitoka katika boma ya ndugu Mathayo Rimba Olemirai wa kijiji cha Majengo huko Arumeru wakati wageni hao walipozuru kijijini hapo kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na serikali ya Uingereza tarehe 9.11.2011
Ndugu Mathayo Rimba Olemirai,mwenye boma akimpatia zawadi ya rungu The Prince of Wales mara baada ya kutembelea boma yake katika kijiji cha Majengo tarehe 9.11.2011.

The Royal Highnesses wakipiga picha na baadhi ya wanakijiji wa Majengo mara baada ya wageni hao kutembelea kijijini hapo tarehe 9.11.2011.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Leganga iliyoko wilayani Arumeru wakiwakaribisha The Prince of Wales na The Duchess of Cornwell kwa kuwapa maua mara tu wageni hao walipowasiri shuleni hapo kukagua miradi inayofadhiliwa na Uingereza tarehe 9.11.2011.
The Prince of Wales akifuatana na Waziri wa Elimu na Ufundi Dr, Shukuru Kawambwa wakiangalia kazi za wanafunzi wa shule ya msingi ya Leganga wakati alipotembelea shuleni hapo tarehe 9.11.2011.
The Prince of Wales akipanda mwembe kama kumbukumbu yake ya kutembelea shule ya Leganga iliyoko katika wilaya ya Arumeru tarehe 9.11.2011.
The Prince of Wales akiangalia chupa ya mvinyo iliyotengenezwa na wajasiriamali wa mkoani Arusha wakati wageni hao walipowatembelea huko Arumeru katika ziara yake ya siku moja tarehe 9.11.2011. PICHA ZOTE  NA JOHN LUKUWI  

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages