Timu hiyo ikikabidhiwa bendera ya taifa leo jijini Dar |
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager imetangaza rasmi kuondoka kwa timu ya Taifa katika mashindano ya ALL AFRICA CUP 2011-BLANTYRE- MALAWI yanayotarajiwa kuanza tarehe 22.11.2011 hadi 26.11.2011.
Akitangaza
safri hiyo, Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema
timu hiyo inaondoka leo kufuatia Bia ya Safari Lager, kukamilisha
mahitaji yote muhimu ya Timu ya Taifa kwa ajili ya safari hiyo na
kukumbusha kwamba bia hiyo ndiyo mdhamini mkuu wa mchezo wa Pool hapa
nchini, na imekuwa ikiidhamini timu ya Taifa ya mchezo wa pool table
tangu mwaka 2008 kwenye mashindano ya Africa na Dunia.
Alisema
ikiwa njiani kwenye Blantyre Malawi, timu itapita katika baadhi ya
mikoa na kucheza mechi za kirafiki na timu za mikoa hiyo ambayo aliitaja
kuwa ni Morogoro, Iringa, Mbeya, Kyela- Mbeya na Kasumulo boarder-
Mbeya na kwamba ni muda mwafaka kwa wananchi kuangalia timu yenu na
kuona jinsi ilivyojiandaa.
Naye kocha mkuu wa timu ya taifa, Denis Lungu aliwataja wachezaji wa timu ya Taifa inayotarajia kuondoka leo.
1
|
OMARY AKIDA - KINONDONI
| ||||
2
|
FELIX ATANAS- DODOMA
| ||||
|
GODFREY MHANDO- KINONDONI
| ||||
4
|
MOHAMED IDDY- KINONDONI
| ||||
5
|
CHARLES VENANCE- TEMEKE- CAPTAIN
| ||||
6
|
ANTONY THOMAS- ILALA
| ||||
7
|
SHAMIS NASSORO- ILALA
| ||||
8
|
ABDALLAH HUSEIN- KINONDONI
|
Akiongelea kuhusu mashindano hayo, Katibu wa chama cha Pool Taifa Bw. Amos Kafwinga alisema, ”Katika
mashindano ya mwaka huu ya ALL AFRICA CUP yanatajiwa kushirikisha nchi
14 wanachama wa ALL AFRICA POOL ASSOCIATION (AAPA) na nchi hizo ni
Africa kusini, Tanzania, Malawi, Zimbabwe, Cameroon, Zambia, Uganda,
Swazland, Reunion FFB, Reunion Arabas, Nigeria , Msumbiji, Morocco na Lesotho.
Akitoa
salam za shukrani kwa Safari Lager kwa niaba ya Chama cha Mchezo wa
Pool Tanzania (TAPA), Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Isaac Togocho
alisema “ Mchezo wa pool table
sasa umekuwa si mchezo tena wa kupoteza muda bali ni mchezo kama michezo
mingine na unaelekea kuwa ajira rasmi kwa vijana wa Tanzania.
Ningependa kutoka shukrani za kipekee kwa Safari Lager na TBL kwa ujumla
kwa kuweza kuiweka Tanzania katika ramani ya michezo kimataifa kupitia
SAFARI LAGER BEER ni fahari kubwa kwa mchezo wa pool table Tanzania.
TAPA inaahidi kuendeleza ushirikiano huu mzuri na mdhamini kwa kusimamia
na kuendeleza mchezo huu wa Pool hapa nchini.”
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)