Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni za GURJAR GRAVURES na GURJAR IMAGES PRIVATE LIMITED
za nchini India Bw. Zainuddin Mahuwala (kulia) akimkabidhi Mbunge wa
Singida mjini Mh. Mohammed Dewji (katikati) hundi ya $ 15,000/= kwa
ajili ya kusaidia jitihada zake za kuboresha Maendeleo katika jimbo lake
la Singida Mjini. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hizo Bw.
Shubair Mahuwala.
Na.Mwandishi wetu.
Mbunge
wa Singida mjini Mh. Mohammed Dewji leo amepokea jumla ya dola za
kimarekani elfu 15 kutoka kwa kampuni ya GURJAR ya India kutokana na
mchango wake katika kutoa huduma kwa jamii hususan kuwasaidia yatima na
watoto ambao wazazi wao hawana uwezo.
Kiasi
hicho cha fedha kimetolewa na kampuni mbili zinazomilikiwa na
Zainuddin R. Mahuwala za GURJAR GRAVURES PRIVATE LIMITED ambayo imetoa
dola 7,500 na GURJAR IMAGES PRIVATE LIMITED ambayo imetoa dola 7,500.
Akipokea
hundi ya fedha hizo Mh. Dewji amesema atazielekeza katika mfuko wa
huduma za elimu wa Mohammed Foundation ambao umekuwa ukisaidia
kuwasomesha watoto zaidi ya 2400 katika jimbo la Singida Mjini.
Wakati
wa makabidhiano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam ofisini kwa Mh.
Dewji, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hizo Bw. Zainuddin Mahuwala ambaye
aliambatana na mtoto wake Shubair Z. Mahuwala ambaye ni Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni hizo, amempongeza sana mbunge huyo na kumtaka
kuendelea na moyo huo wa kusaidia jamii huku akimuombea Mungu
amzidishie.
Mh.
Dewji amekuwa akipigania kupatikana kwa fursa sawa ya elimu kwa watoto
Singida mjini ikiwemo kujitolea kukarabati na kujenga shule sambamba
na kununua vifaa vya elimu. Kwa sasa Mh. Dewji anasomesha watoto zaidi
ya 2400 yatima na ambao wazazi wao hawana uwezo ili nao wapate nafasi
ya kupata elimu itakayowasaidia kujikomboa katika maisha.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)