TANZANIA
imesimamia msimamo wake wa kuitosa Uingeereza iliyoweka masharti kwa
nchi zinazotaka misaada yake ziruhusu vitendo vya ushoga na kuruhusu
kuhararisha ndoa za jinsia moja. Akizungumza wakati wa mkutano
na waandishi wa habari, Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe , alitoa
msimamo huo leo Jijini Dar es Salaam akisema huko ni kwenda kinyume na
sheria na utamaduni wa nchi yetu inayotambua ndoa ya mme na mke kama
kiini cha familia.
Membe
alisema hayo yaliyotokana na mkutano wa Jumuia ya Madola uliofanyika
wiki iliyopita Perth, Australia, ambapo alitoa msimamo huo kufuatia
kauli ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron kuwa wana mpango wa
kusitisha misaada kwa nchi ambazo katiba na sheria zake hazitambui
mashoga na ndoa zao.
Aidha Waziri Membe aliwaambia waandishi wa habari kuwa tamko hilo ni msimamo wa chama cha Conservative na kibaya zaidi linatoka Uingereza ambako ndio wenye Jumuia ya Madola hivyo linaweza kusababisha kuvunjika kwake na Cameroun na nchi hiyo ndio watawajibika jumuia hiyo ikivunjika.
Alisema miongoni mwa nchi 54 za Jumuia ya Madola kati yake nchi 13 ushoga ni sehemu ya katiba yao wakati 41 hazina utamaduni huo hivyo msimamo wa Tanzania ni kuwa na ndoa za jinsi mbili tofauti, kinyume na hapo unafungwa kifungo miaka 30.
Alisema kuendelea kukumbatia ushoga si jambo zuri na si la kulishabikia hata kidogo vinginevyo wanaweza kujuta nchi ikijihusisha na ushoga na kuukubali kupata misaada ya maendeleo.
"Tanzania hatuwezi kuyumbishwa kwa masharti ya kipuuzi bora tuitunze nchi yetu. Tanzania ni nchi maskini lakini kamwe haturuhusu kuingiliwa na nchi nyingine. Kama ndio hivyo basi wakae na hela zao," alisema Waziri Membe wizarani kwake.
Alisema katika mkutano wa Madola, walijadili mabadiliko ya hali ya hewa ambapo walibainisha nchi zinazotegemea mvua zichukue hatua gani kuishi bila kuathiri hali hali ya hewa. Pia alisema walijadili kuhusu hatua za kuchukua ili kuvisaidia visiwa vidogo kama Maldives vinavyoliwa na maji ya bahari yanayojaa kufuatia mabadiliko ya hali ya hewa.
Alisema watakuwa na mkutano London Aprili mwakani kujadili mikakati hiyo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)