Trafiki Polisi akiongoza magari katika junction kubwa ya Ubungo, maarufu kama Ubungo Mataa.
Fuso ikiwa imeingia katika moja ya mtaro mkubwa ulioko bara bara ya Ubungo karibu na Ubungo mataa.
Kwa kipindi kirefu sasa eneo la Ubungo karibu na Mataa ya kuongozea magari yanayo ingia Jijini au yale
yanayotoka pande mbili, mengine yakitokea Mwenge na mengine yakitoke
Buguruni na kwenda sehemu mbali mbali za jiji limevamiwa na wafanya
biashara ndogo ndogo maarufu kama Wamachinga.
Nimejaribu
kulifuatilia kwa kipindi kirefu ili kuweza kujiridhisha kujua kama
wamepewa ruhusa na nani kufanya biashara katika eneo lisilo rasmi,
nilijaribu kuongea na wamachinga wachache; wa kwanza anaitwa Salum
Ramadhan anauza taa za kichina katika eneo hilo,
yeye alidai hawajaruhusiwa na mtu kufanya biashara hapo ila ni kutokana
na ugumu wa maisha ndio umewapelekea kufanya biashara katika eneo hilo
na wa pili naye Ndg. Deogratius Shirima akasema maneno hayo hayo ambayo
hayapishani maana na huyu wa kwanza.
Sikuishia hapo nikataka kujua je kuna
mtu yeyote ambaye anakuja kukusanya japo ushuru kutoka kwao? nao kwa
pamoja wakasema kuna mtu huwa anakuja kukusanya ushuru lakini wao hawana
uhakika kama ni kutoka Serikali za mitaa au la! nikawauliza swali
jingine, huyu jamaa ambaye ameweka jenereta hapa na kuwapa huduma ya
Umeme mnamlipa Sh. ngapi? wakasema kila taa 1 ni Sh. 1000/- nikapenda
nijue sasa swali langu la msingi, wanajua HATARI
iliyo mbele yao kutokana na kufanya biashara kando kando ya bara bara
kubwa kama hii ambayo inapitisha magari mengi na hasa mengine yanakuwa
yako kwenye mwendo wa kasi! wakasema wanaifahamu ila hawana jinsi
wataenda wapi na maisha yenyewe ni magumu!
Kwa kweli nilitoka bila kuwa na jibu sahihi nini hatma yao kama gafla gari likitoka kwenye bara bara na kuwavama.
Tatizo
hili naamini serikali wanaliona ila wanalifumbia macho na pindi ajali
itakapo tokea ndio wanafumbua macho na kujua sehemu sio halali, ni vema
serikali ikalichukulia hatua mapema kabla halija tokea la kutokea.
Tumekua tukiona sehemu mbali mbali ajali zinatokea na kuua watu wengi
ambao wapo kando kando ya bara bara kwa hiyo ni vema Serikali ikachukua
tahadhari mapema.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)