Tamasha la Str8t Music inter College Lafana Jijini Dar es Salaam - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Tamasha la Str8t Music inter College Lafana Jijini Dar es Salaam


Mkali wa Hip hop kutoka nchini Marekani,Fabolous akishusha mistari ya nguvu mbele ya umati mkubwa (haupo pichani),uliofika kumshuhudia kwenye viwanja vya Lidas juzi usiku
Kijana mdogo,lakini matata kwa michano huru,huyu ni mmoja washindi wa Michano huru kutoka Mkoani Mbeya akionesha umahiri wake kwenye tamasha la Str8t Muzik Inter-College Festival 2011 lililofanyika juzi Usiku katika viwanja vya Lidaz club,Kinondoni jijini Dar.
Afande Sele akiimba kwa hisia jukwaani
Mmoja wa wasanii mahiri kutoka THT,Barnaba akitumbuiza jukwaani usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Str8t Muzik Inter-College Festival 2011 lilifanyika usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Lidaz club,Kinondoni jijini Dar.
Baadhi ya wasanii mahiri wa hip hop kutoka kundi la Wateule,Jay Mo na Mchizi Mox wakitumbuiza kwenye tamasha la Str8t Muzik Inter-College Festival 2011 lililofanyika juzi usiku katika viwanja vya Lidaz club,Kinondoni jijini Dar,ambapo mashabiki kibao walifurika na kujiachia vilivyo
Umemcheki pande ya mtu hii..! hapa alikuwa akitazama usalama wa msanii Fabolous kablA ya kupanda jukwaani.
Gwangwe Mob Wakifanya Vitu vyao chini ya inspector Haroun
Kikundi cha Wanaume
THT
Dj Zero kutoka Clouds FM,akiangusha ngoma moja baada ya nyingine,ile mzuka safi kabisa.
Sehemu ya mashabiki wakifuatilia tamasha hilo kupitia screen kubwa zilizokuwa zimefungwa viwanjani hapo.Picha Zote na Ahmed Michuzi

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages