Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
na ujumbe wa Serikali yake leo, Jumapili, Novemba 27, 2011, amekutana
na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA).
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam,
yamefanyika katika mazingira ya urafiki na ujumbe wa CHADEMA
umewasilisha mapendekezo yake kuhusu mchakato wa kuandika Katiba Mpya
ya Tanzania. Serikali imepokea mapendekezo hayo.
Hata
hivyo, pande zote mbili zimekubaliana kukutana tena asubuhi ya kesho,
Jumatatu, Novemba 28, 2011, ili kuipa nafasi Serikali iweze kutafakari
mapendekezo hayo.
Lakini pande hizo
mbili zimekubaliana kuwa Katiba ya sasa ni Katiba nzuri iliyolilea
Taifa kwa miaka 50 iliyopita kwa sababu ni Katiba ya sasa
iliyoliwezesha Taifa la Tanzania kuwa na amani, utulivu na kupata
maendeleo makubwa ambayo nchi yetu imepata mpaka sasa.
Pia pande zote
mbili zimekubaliana kuhusu umuhimu wa kutunga Katibu Mpya kama
Mheshimiwa Rais Kikwete alivyoliahidi taifa wakati wa salamu zake za
mwaka mpya Desemba 31, mwaka jana, 2010, Katiba ambayo italiongoza
Taifa la Tanzania kwa miaka mingine 50 ijayo.
Katika mazungumzo
hayo, Mheshimiwa Rais aliwahakikishia wajumbe hao wa CHADEMA
wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Mheshimiwa Freeman Mbowe kuwa
ni dhamira yake na ya Serikali yake kuhakikisha kuwa Tanzania inapata
Katiba mpya.
Katika mkutano huo, pande zote mbili
zimekubaliana kuwa ni jambo muhimu sana kwa mchakato mzima wa kutungwa
kwa Katiba Mpya kuendeshwa kwa namna ya kulinda na kudumisha tunu za
taifa za amani, utulivu na umoja wa kitaifa.
Aidha, pande zote
mbili zimekubaliana kuwa mchakato huo uendeshwe kwa kuzingatia misingi
ya mambo mengine muhimu kwa taifa la Tanzania kama vile kujiepusha na
vitendo vya uvunjifu wa amani, kuligawa Taifa kwa misingi ya udini na
ukabila ama kutugawa kwa misingi ya maeneo.
IMETOLEWA NA:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
NOVEMBA
27, 2011
DAR ES SALAAM
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigana na
Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akigana na Mheshimiwa John Mnyika Mbunge Jimbo
la Ubungo CHADEMA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigana na
Mheshimiwa Arfi Mbunge wa CHADEMA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na
Kiongozi wa CHADEMA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisikiliza maelezo
toka kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe baada ya kupokea
mapendekezo ya chama hicho juu ya kuundwa katiba mpya yatayozungumzwa
kwenye mkutano huo wa kihistoria uliofanyika jana Ikulu jijini Dar es
salaam
Rais Jakaya Kikwete Akifurahi jambo na
Viongozi wa Chadema wakiongo Wa Chadema
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na uongozi
wa CHADEMA katika mkutano huo wa kihistoria
Mh. Tundu Lissu akikoroga chai baada ya
mkutano huku Profesa Baregu naye akijiandaa kujisevia
Rais Jakaya Kikwete akiongea na wageni wake
Rais Jakaya Kikwete akimpa juisi Mwenyekiti wa
CHADEMA Mh Freeman Mbowe baada ya mkutano
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiendelea kupata
Vinywaji na Viongizi Waandamizi wa CHADEMA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigana na Profesa
Mwesiga Baregu CHADEMA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigana na
Mheshimiwa Tundu Lissu Mbunge Jimbo la Singida Mashariki CHADEMA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigana na Profesa
Abdallah Safari CHADEMA
Kwa Kuona Picha Zaidi <<< BOFYA HAPA >>>
Picha Zote na IKULU
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)