Makamu
wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba yake wakati wa Tamasha la wakati wa Tamasha la Vijana la
‘Tunaimani kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi’ lililofanyika kwenye
Viwanja vya Don Bosco Upanga jijini Dar es Salaam leo Novemba 9, ikiwa
ni sehemu ya maandalizi ya vijana hao kuelekea Durban kushiriki katika
Mkutano wa 17 wa Mabadiliko ya Tabia nchi unaotarajiwa kufanyika
mwishoni mwa mwezi huu, Afrika ya Kusini.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisaini tamko la Viongozi wa dini kuhusu mabadiliko ya Tabia Nchi,
wakati wa Tamasha la Vijana la ‘Tunaimani kuhusu Mabadiliko ya Tabia
Nchi’ lililofanyika kwenye Viwanja vya Don Bosco Upanga jijini Dar es
Salaam leo Novemba 9, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya vijana hao
kuelekea Durban kushiriki katika Mkutano wa 17 wa Mabadiliko ya Tabia
nchi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu, nchini Afrika ya
Kusini. Kushoto ni Askofu Mkuu wa Jimbo la Tabora na Mwenyekiti wa
Viongozi wa Dini Nchini, Askofu Paul Ruzoka
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi Tamko la Viongozi wa Dini kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi,
Askofu Mkuu wa Jimbo la Tabora na Mwenyekiti wa Viongozi wa Dini Nchini,
Askofu Paul Ruzoka, baada ya kusaini tamko hilo wakati wa Tamasha la
wakati wa Tamasha la Vijana la ‘Tunaimani kuhusu Mabadiliko ya Tabia
Nchi’ lililofanyika kwenye Viwanja vya Don Bosco Upanga jijini Dar es
Salaam leo Novemba 9, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya vijana hao
kuelekea Durban kushiriki katika Mkutano wa 17 wa Mabadiliko ya Tabia
nchi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu, Afrika ya Kusini.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Fatuma Mussa, mwakilishi wa Tanzania ambaye ni miongoni
mwa vijana watakaoelekea Durban katika mkutano wa 17 wa Mabadiliko ya
Tabia nchi unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi huu nchini Afrika ya
Kusini. Makamu alikuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Vijana la
‘Tunaimani kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi’ lililofanyika kwenye Viwanja
vya Don Bosco Upanga jijini Dar es Salaam leo Novemba 9
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa dini na vijana
kutoka mataifa 13 wanaokwenda kushiriki katika Mkutano wa Mabadiliko ya
Tabia Nchi unaofanyika Durban nchini Afrika ya Kusini mwishoni mwa mwezi
huu. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu Wa Rais
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)