WAFUASI WA CHADEMA WALIVYOWAPOKEA KWA SHANGWE NA VIFIJO WABUNGE WAO WALIOWEKWA RUMANDE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WAFUASI WA CHADEMA WALIVYOWAPOKEA KWA SHANGWE NA VIFIJO WABUNGE WAO WALIOWEKWA RUMANDE



Wanachama wa CHADEMA mjini Igunga, jioni hii walijawa na furaha kubwa wakati wakiwa wanawapokea wabunge wao waliokamatwa hivi karibuni na kuwekwa rumande mjini Igunga na baadae kuhamishiwa kituo cha polisi mkoani Tabora kwa kosa la kumsukasuka mkuu wa Wilaya ya Igunga Fatuma Kimario. Wabunge hao ni Sylivester Kasulumbai, mbunge wa Maswa Mashariki, Suzani Kiwanga, ambae ni mbunge wa viti maalumu. Mwingine ni kada wa chama hicho. Kwa pamoja wamepata dhamana na kesi yao itatajwa tarehe 12.10.2011. Pichani wakiwa katika maandamano jioni hii mjini Igunga. Picha na Victor Makinda.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages