Mkurugenzi wa
Makosa ya Jinai Robert Manumba akitoa taarifa kwa vyombo vya habari
mchana huu, katika mkutano na waandishi wa habari juu ya wafanyabiashara
wanaojihusisha na kuficha sukari nchini, mkutano huo umefanyika makao
makuu ya jeshi la polisi nchini.
---
1.
Awali ya yote napenda niwashukuru kwa kazi
nzuri mnayoifanya ya kuelimisha jamii kuhusu mambo mbalimbali ya
maendeleo na hasa suala la kuzuia na kukabiliana na uhalifu hapa
nchini.
2. Jambo kubwa lililoko mbele yetu ni wimbi la kuongezeka kwa
uhaba wa sukari hapa nchini, ambapo utafiti umeonyesha kuwa uhaba huo
umesababishwa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kuhodhi
bidhaa hiyo ili kusababisha upungufu sokoni.
3. Utafiti pia umeonyesha kuzuka kwa soko la bidhaa hiyo kwenye
nchi jirani, hivyo wafanyabiashara wasio waaminifu kwa kuvutiwa na bei
kubwa katika masoko hayo kuanza kuvusha sukari kinyume cha sheria na
kwenda kuiuza nchi za jirani.
4. Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na taasisi zingine
kama vile TRA, Bodi ya Sukari, Uhamiaji, Wizara ya Biashara, TBS, Fair
Competition Board, Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali na TISS,
limeandaa oparesheni maalum ili kuhakikisha kwamba sukari inapatikana
kwa kiwango cha kuridhisha katika soko la ndani na kwa bei elekezi
iliyokubaliwa na wadau wote husika.
5. Tunawaonya wafanyabiashara wote wanaojihusisha na kuficha,
kusafirisha sukari nje ya nchi kinyume cha sheria ama kuuza sukari hiyo
kinyume na bei elekezi waliyokubaliana kuacha tabia hiyo mara moja,
yeyote atakayekaidi na kuendelea kufanya uhalifu huo atakamatwa na
hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi yake.
6. Tunawaomba wananchi wote
kutuunga mkono ili kuhakikisha kwa pamoja tunakomesha tabia hii ya
wafanyabiashara wachache wasio waaminifu wanaojihusisha na biashara za
magendo hata katika bidhaa zingine
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)