Salaam,Shikamoo wakubwa na vijana wenzetu mambo vipi?
kwanza kabisa tunapenda kuwashukuru Mabloga wote popote Duniani kwa
kuendelea kutusaidia kwa kiasi kikubwa sana kutufikishia ujumbe wetu
pale tunapo omba kusaidiwa,Baada ya shukrani hizo za kipekee kabisa,Pia
tunapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wale wanavyuo,watumishi wa
vyuo na wadau wote ambao wameendelea kuipa sapoti kubwa website ya MATUKIO NA
WANAVYUO.
Ili kuendeleza kuwaunganisha wanavyuo wote Tanzania
na kuwakutanisha na wanavyuo wengine ambao ni watanzania lakini
wanasoma nje ya nchi tumeamua sasa kuwaletea njia mbadala ambayo
itawaunganisha kirahisi kabisa nayo ni Socilal
network. Hivyo basi kwa heshima na taadhima tunapenda kuwatambulisha
kwenu kiunganishi kipya kabisa ambacho kinakwenda kwa jina la UNIVERSITIES
CONNECTS .na Jina la tovuti ni www.tzuniversitiesconnects.tk
Katika website hii maalum kabisa wanavyuo na wanafunzi mbalimbali
pamoja na wadau wataweza kukutana humo, kubadirishana mawazo ya kisomi
zaidi na kufahamiana zaidi ikiwa ni pamoja na kupata mawazo mapya, pia
wataweza kupata marafiki wapya na kama haitoshi kuna Visual Discussion
Room ambapo wataweza weka Mada mbali mbali na kuijadili moja kwa moja,
na zaidi ya yote utapata nafasi ya kuchati muda wowote.
Pia kwa
kuzingatia kuwa wanafunzi wengi wanatumia Mobile phones, basi kupitia
Mtandao huu utaweza pia kutumia simu yako ya mkononi kuendelea
kuwasiliana. Ni matumaini yetu ya kwamba mtandao huu wa kipekee na mpya
kabisa utaenda kukuunganisha wewe na mwenzako... Tunaomba ukipata
taarifa hii umwambie na mwenzako pia ajiunge ni Bure kabisa.
Tunatanguliza Shukrani zetu asanteni sana.
Sisi,Matukio na wanavyuo Crewtwanavyuo@live.com
ILI KUJIUNGA MOJA KWA MOJA BOFYA HAPA CHINI
UNIVERSITIES CONNECTS-YOUR HERE BECAUSE YOU DESERVE
Sisi,Matukio na wanavyuo Crewtwanavyuo@live.com
ILI KUJIUNGA MOJA KWA MOJA BOFYA HAPA CHINI
UNIVERSITIES CONNECTS-YOUR HERE BECAUSE YOU DESERVE
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)